JAJI MARAGA akutana na “Kaa La Moto” baada ya Kutoa Salamu za Pole kuptia Twitter !

Baadhi wa Wakenya wamemkemea vikali Jaji Mkuu (CJ) David Maraga kuhusiana na kuachiliwa huru kwa washukiwa wa ugaidi wanaoshukiwa kuhusika na shambulio la 2013 Westgate lililosababisha vifo vya watu 71.

Raia hao wa Kenya ambao bado wapo katika Majonzi mazito kuhusu uvamizi uliotokea Jumatano, Januari 15, katika Hoteli ya DusitD2,  wamemshambulia Jaji Maraga kwa madai ya kukosa kutoa uongozi unaofaa katika idara ya Mahakama

Hasira za Wakenya kupitia Twitter zilijiri baada ya Maraga kutuma ujumbe wa pole kwa walioathirika kwa njia moja au nyingine kufuatia shambulio la eneo la 14 Riverside. Kulingana nao, kuachiliwa huru kwa washukiwa wa ugaidi uliofanyika Westgate siku moja kabla ya shambulio la juzi ni ishara ya kufeli kwa idara yake.

“Naungana na Wakenya katika kukashifu uvamizi uleotokea Riverside jana (Jumanne). Risala zangu za rambirambi ziwaendee familia zilizopoteza wapendwa wao, na afueni ya haraka kwa waliojeruhiwa. Nawapongeza maafisa wetu wa usalama na wengine wote waliosaidia kukabiliana na hali hiyo. Mungu ibariki Kenya,”  CJ aliandika kupitia Twitter. Kulingana na jumbe nyingi za Wakenya, ujumbe wa CJ haukupokelewa vyema kwani alikumbushwa kuhusu kuachiliwa huru kwa mshukiwa wa ugaidi siku moja kabla ya shambulio katika Hoteli ya Dusit lililosababisha vifo vya watu 21 na wengine 28 kulazwa hospitalini kwa majeraha mbalimbali

Related posts