NAY TRUE BOY amefafanua Kuhusu Kumwagia watu MAJI kwenye Show Zao !!

KUMEKUWA na maswali mengi tu ya Chini chini ambayo yameambatana majibu ya kuhisi kutoka kwa baadhi ya wadau na mashabiki wamuziki wa Kizazi kipya Nchini Tanzania, kuhusu Kitendo cha Wasanii NAY WA MITEGO na DIAMOND PLATNUMZ kumwagia maji mashabiki wao wakati waki-perform katika majukwaa yao

Hii imekuwa ni mara kwa mara ambapo Nay “The True Boy” ndiye anadai kuanzisha utaratibu huo katika matamasha mbali mbali na kisha Diamond kuanza kufanya hivyo kipindi hicho, lakini hakukuwa na maswali kama ambayo tunakutana nayo sasa hivi

Waungwana walianza kuhusisha kitendo hicho na imani za “Kishirikina” ikiwa ni baada ya Diamond kufanya hivyo katika Tamasha lake la “WASAFI FESTIVAL” ambalo lilizunguka katika mikoa kadha wa kadha hapa Nchini Tanzania.

Nay ambaye hivi sasa anafanya vizuri na Wimbo wake mpya wa MBELE KWA MBELE, amekiri kukutana na Maoni hayo kutoka kwa mashabiki zao, na ametolea ufafanuzi kuwa, kitendo cha kumwagia Maji mashabiki sio cha kishirikina au kuvuta watu kwenye Show zao, bali ni maji ya Baraka, na kuwamwagia vile, ni kama kuamsha “mizuka ya Burudani” kama ambavyo mtu akifanya kazi akachoka, basi huoga ili kuupa Mwili Nguvu

MSIKILIZE HAPA :

Related posts