MARUFUKU kuvaa Mavazi Yenye Rangi NYEKUNDU Uganda

WATU watakaobainika kuwa wamevaa Nguo Nyekundu, Kofia Nyekundu na Kitambaa chekundu Katika wilaya ya LAMWO nchini Uganda, watakiona “cha Mtema Kuni” kutoka kwa jeshi la Polisi maana watakuwa wanaashiria kuunga mkono chama cha People’s Power.

Agizo hilo limetoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, (RDC) James Nabinson Kidega ambaye amelipatia mamlaka Jeshi la polisi Katika wilaya hiyo kuhakikisha kuwa linakamata Mavazi hayo ambayo yanauzwa ama kupatia watu ambao wanamuunga Mkono Msanii wa Uganda ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kama “Bobi Wine”

Tofauti na hilo, Bw. Kidega ameongeza kuwa, Jeshi la Polisi pia lina mamlaka ya kumkamata Raia yeyote wa Wilaya yake ambaye atakuwa amevalia ama Nguo Nyekundu, Kofia Nyekundu ambazo zina kiashiria cha kuunga mkono chama hicho cha People’s Power kinachoaminiwa kuwa kipo kinyume na matakwa ya Serrikali ya Rais Yoweri Museveni.

Naye Kamanda wa Polisi katika Wilaya ya Lamwo Nchini Humo , Eliau Osega amekiri kupokea agizo hilo kutoka kwa Mkuu wake wa Wilaya, lakini akakiri kuwa litakuwa ni zoezi gumu ambalo huenda lisiwezekane kutokana na jeshi hilo kumtia nguvuni mtu kwa sababu ya mavazi yake kwa sababu kila mmoja ana haki ya kuvaa vazi ambalo anadhani linamfanya awe huru na linamfanya awe na muonekano Mzuri

Hata Hivyo, Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Katika Wilaya ya Lamwo ambaye pia ni Mchambuzi wa masuala ya Kisiasa Nchini Uganda, James Ochola, amesema kuwa agizo la Mkuu wa Wilaya sio sahihi maana kila Raia ana haki ya kuvaa Mavazi anayostahili kuvaa

 

Facebook Comments

Related posts