KUNGUNI WAFUNGA MAHAKAMA !

MAHAKAMA ya jimbo la ROGERS, Oklahoma Nchini Marekani, imelazimika kusitisha Shughuli za Kimahakama baada ya kubainika kwa Kunguni ndani ya Mahakama Hiyo

Kunguni hao walionekana wakidondoka kutoka katika Moja ya Vazi la Mwanasheria aliyekuwa katika Mahakama hiyo wakati shughuli za kimahakama zikiendelea, hli iliyosababisha Uongozi kuchukua Jukumu la kufunga mahakama mpaka hali itakapokuwa Sawa.

Akifafanua kuhusu hali hiyo, Mmoja wa Viongozi katika utawala wa Jimbo hilo ambaye pia alipewa jukumu la kutoa ufafanuzi juu ya hatua hiyo, SCOTT WALTON ameweka bayana kuwa mwanasheria huyo alifika katika Ghorofa ya Tatu ambako ndipo kilipo Chumba cha Mahakama huku Kunguni hao wakidondoka kutoka katika Vazi lake, hali iliyozua utata wa kuenea kwa Wadudu hao hatarishi.

Mahakama ya Jimbo La ROGERS, Jijini Oklahoma, Marekani

Hebu Vuta picha kwamba mtu hafahamu kuwa katika Vazi lake kuna Kunguni. Lakini tulipewa taarifa kuwa, Kunguni walionekana wakiwa katika moja ya MAKBLASHA ya Viongozi wa Mahakama. na Kama unavyojua, wale wadudu husambaa kwa kasi sana” alisema WALTON

Hata Hivyo, Mahakama imefungwa ili kuhakikisha wadudu hao wanaondolewa Haraka Iwezekanavyo

Related posts