RAIS WA SUDAN : ” MILANGO IKO WAZI KWA WAANDAMANAJI KUFANYA MAZUNGUMZO”

Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesema mlango wa mazungumzo utaendelea kuwa wazi kwa waandamanaji vijana ambao wanaingia mitaani kuandamana kwa Madai ya hali mbaya ya uchumi na kutumia mgogoro wa Sudan Kusini kama chanzo kikuu cha mgogoro wa kiuchumi nchini Sudan.

Al-Bashir amebainisha kuwa, Mgogoro wa Sudani Kusini ni sababu kubwa ya kuzorota kwa uchumi wa Sudan.

Sudan imekuwa ikisumbuliwa na migogoro katika historia yake licha ya makubaliano ya amani uliosainiwa mwaka 2015. Serikali za kusini zilisalia na kuunda Jamhuri ya Sudan Kusini mwaka 2011.

Tangu Desemba 19 mwaka 2018, maeneo kadhaa nchini Sudan ikiwemo mji mkuu Khartoum imekuwa ikishuhudia maandamano ya wananchi wakilalamikia hali mbaya ya uchumi na bidhaa kupanda bei

Related posts