WMO Wathibitisha Kuwa Viwango vya Joto Vinapanda

Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa duniani, WMO limesema ongezeko la viwango vya joto ni ishara ya wazi ya mabadiliko ya tabia-nchi ya muda mrefu, huku wakifafanua kuwa miaka minne iliyopita viwango vilikuwa vya kipekee.

WMO katika taarifa imesema miaka katika ya 2015, 2016, 2017 na 2018 kumekuwa na Joto Kubwa na hiyo ni ishara ya wazi kuwa mabadiliko ya tabia-nchi yanaendelea.

Akizungumzia mwenendo wa hali ya hewa, Katibu Mkuu wa WMO, Petteri Taalas amesema mwenendo wa muda mrefu ni muhimu kuliko uchunguzi wa mwaka mmoja mmoja na kwamba taswira inaonyesha kuwa viwango vya joto vinapanda.

“miaka 20 iliyokuwa na joto jingi zaidi imekuwa miaka 22 iliyopita. Viwango vya joto katika kipindi cha miaka minne iliyopita vimekuwa vya aina yake nje na ndani ya bahari”. Alifafanua

Taalas amesema viwango vya joto ni kiungo tu kwenye taswira nzima kwani  athari  kubwa na mbaya zinazotokana na hali ya hewa viliathiri nchi nyingi na mamilioni ya watu na kusababisha athari mbaya kwenye uchumi na mazingira mwaka 2018. Kati ya athari mbaya za ongezeko la joto duniani ni njaa, ukame, mafuriko na kuongezeka kina cha bahari na hivyo kuangamiza idadi kubwa ya visiwa na maeneo ya pwani.

Related posts