YOGO BEATS : “UKINILIPA VIZURI, NITAFANYA KAZI YAKO” (AUDIO)

SINA hakika kama kuna mtu ambaye atakidhi kiu yako kiufasaha zaidi hasa katika Nyanja ya Kazi, kama utampa malipo ambayo hayaridhishi hata kidogo, na hiyo ipo kwa Watu Wengi Sana

Wengi tulianza kumuelewa Zaidi Producer YOGO BEATS baada ya kuanza kufanya Kazi na NEDY MUSIC kupitia Tracks kadha wa kadha hasa ikiwemo NISHALEWA na ONE AND ONLY. Tofauti na hilo, Ndiye Producer ambaye amemfanya Msaii huyo kujipatia Tuzo ya kimataifa ambayo imemuweka katika Ramani Nzuri sana ya Muziki wa kimataifa

Tofauti na Producers wengine, YOGO BEATS hana njaa ya kutengeneza kazi nyingi ili awe na sifa ya kutengeneza kazi nyingi sana, ila yeye amejikita katika kutengeneza Kazi chache ambazo zina ubora wa kumpatia Historia nzuri katika Ulimwengu wa Muziki, na ndio maana Husikii sana kazi zake Nyingi.

Lakini Pia, Yogo Beats ndiye ambaye amesuka Mkwaju mpya wa Msanii Ommy Dimpoz unaoitwa “NI WEWE” na bado unazidi kufanya Vizuri, licha ya kuwa waliufanya katika kipindi kigumu ambacho Ommy Dimpoz hakuwa sawa kiafya.

Sasa, kuhusu kufanya Kazi, Yogo ameweka bayana kuwa, Kama msanii atamlipa Malipo Mazuri ya kuiridhisha, basi lazima amfanyie kazi Nzuri, maana pia kuna njia mbali mbali za kumalizaana Kimalipo

MSIKILIZE

Related posts