Kiongozi wa Korea Kaskazini ajitokeza.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza baada ya kutoonekana kwa kipindi kirefu, huku kukiwa na uvumi kwamba huenda kiongozi huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo.
Taarifa zilizotolewa na Shirika la Utangazaji la Korea Kaskazini (KCNA) zimemuonesha kiongozi huyo akikata utepe kuzindua kiwanda cha mbolea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).
Kim hakuwa ameonekana hadharani tangu alipozungumza na wananchi katika hotuba ya kitaifa iliyorushwa na vyombo vya habari Aprili 12 mwaka huu.
Baadhi ya nchi hasa za Magharibi zimechukulia ukimya huo kudhania kwamba kiongozi huyo anaumwa huku ikisadikiwa kuwa timu ya madaktari kutoka China ilienda nchini mwake kumtibu.

Related posts