Serikali kufanya Tathimini ununuzi wa zao la Pamba

Serikali imesema inafanya tathmini ya hali ya ununuzi wa zao la Pamba katika msimu wa mwaka 2019 ili kuondoa changamoto zilizojitokeza kabla msimu mpya wa ununuzi kuanza mwaka huu.
Akizungumza na viongozi wa wilaya ya Chato mara baada ya kutembelea Viwanda vya kuchambua pamba, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo GERALD KUSAYA amesema msimu mpya wa ununuzi utatangazwa mara baada ya tathmini ya msimu uliopita kufanyika.
KUSAYA amesema kabla msimu haujafunguliwa serikali itahakikisha inalipa madeni ya Wakulima, Wanunuzi na Ushuru wa AMCOS, Halmashauri pamoja na Mfuko wa Pembejeo.
Aidha Katibu Mkuu KUSANYA amekitaka Chama Kikuu cha Ushirika Chato-CCU, kuwahamasisha wakulima kuzalisha zaidi zao la pamba ili ipatikane malighafi za kutosha kutumika kwenye kiwanda chake cha kuchambua pamba.
Ametoa wito huo kufuatia taarifa ya Meneja Mkuu wa Chama hicho JOSEPH MASINGIRI ambaye alisema kiwanda kimeshindwa kuendelea na uchakataji marobota kutokana na uhaba wa pamba katika msimu uliyopita wa mwaka 2019.

Related posts