WANAJESHI 9 WA UGANDA WAWEKWA KARANTINI

Askari tisa wa Kikosi cha Ulinzi cha Wananchi wa Uganda (UPDF) kilichopo nchini Somali wametengwa baada ya kugundulika kwa askari mmoja kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Kwa mujibu wa gazeti la Daily monitor la nchi hiyo siku ya Jumatano jioni, UPDF ilithibitisha kuwa askari wao huyo aliyepo katika majeshi ya muungano wa Jumuiya ya Afrika nchini Somalia (AMISOM) alipimwa na kuthibitika kuwa na ugonjwa wa COVID-19 na alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu. UPDF imesema kwamba askari huyo alionyesha kuwa na dalili za mafua na kikohozi na kuwa anaendelea vizuri…

Read More

VICTORIA KIMANI : “Huu Ni Muda wa Kuipa Nafasi Digitali”

Katika Ulimwengu wa Burudani, Wasanii mbali mbali na wadau husika wamekuwa katika wakati mgumu hasa kiuchumi kutokana na Kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona. Hii inatokana na ushauri wa Wataalamu wa Afya na Viongozi mbali mbali Duniani kusihi watu kuepukana na Mikusanyiko ya Watu ili kuzuzia kusambaa kwa Virusi hivyo. Nchini Kenya, hivi sasa hakuna matamasha ya Burudani kama ilivyokuwa awali, na hii inatokana na agizo la Serikali ya Nchi hiyo kuwasihi watu kutulia Nyumbani na kuepusha misongamano ya Watu katika maeneo mbali mbali. Victoria Kimani, mmoja kati ya…

Read More

KOCHA WA ZAMANI WA TOTTENHAM ATAMANI KURUDI KLABUNI HAPO.

Meneja wa zamani wa timu ya soka ya Tottenham ya nchini Uingereza Mauricio Pochettino amesema kuwa ana imani siku moja atarejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani ambayo aliachana nayo mwezi November 2019. Kocha huyo raia wa Argentina imeripotiwa kuwa ni miongoni mwa makocha waliowahi kufanya vizuri katika klabu hiyo hasa ikizingatiwa kuwa mwaka jana alifanikiwa kuifikisha katika fainali ya Ligi ya Mabingwa barani ulaya ambapo alipoteza kombe hilo dhidi ya Liver pool. Kwa sasa kocha huyo anatajwa kuwa katika malengo ya wamiliki wapya wa timu ya New Castle wanaotajwa…

Read More