KOCHA WA ZAMANI WA TOTTENHAM ATAMANI KURUDI KLABUNI HAPO.

Meneja wa zamani wa timu ya soka ya Tottenham ya nchini Uingereza Mauricio Pochettino amesema kuwa ana imani siku moja atarejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani ambayo aliachana nayo mwezi November 2019.

Kocha huyo raia wa Argentina imeripotiwa kuwa ni miongoni mwa makocha waliowahi kufanya vizuri katika klabu hiyo hasa ikizingatiwa kuwa mwaka jana alifanikiwa kuifikisha katika fainali ya Ligi ya Mabingwa barani ulaya ambapo alipoteza kombe hilo dhidi ya Liver pool.

Kwa sasa kocha huyo anatajwa kuwa katika malengo ya wamiliki wapya wa timu ya New Castle wanaotajwa kuamsha matumaini mapya ya timu hiyo

Pochetino anaamini siku moja atarudi kuja kumalizia kazi iliyobaki ya kuipa taji timu hiyo ingawa hajafahamu itakuwa lini.

Related posts