ZITTO AMJIBU MAKONDA

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amemjibu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kufuatia kauli yake ya kuwapa saa 24 wabunge wote waliopo katika mkoa huo.

Makonda amesema atakaye ruhusiwa ni yule mwenye kibali cha Spika. – “Mimi ni Mbunge wa Kigoma Mjini, nipo Dar sijakwenda Dodoma Bungeni sababu ninaamini kuwa Bunge lilipaswa kuahirishwa ili kupambana na Korona, sitakwenda Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hana Mamlaka yeyote ya kuniamulia niwe wapi katika Jamhuri ya Muungano” “Sitakwenda Dodoma, nitakaa Dar es Salaam kwa uhuru kabisa, najilinda dhidi ya korona mimi binafsi na familia yangu ninakaa nyumbani, ninawalinda wapiga kura wangu wa Kigoma mjini pia, haya masaa 24 aliyotoa Mkuu wa Mkoa yaishe kwa Wabunge ni UPUUZI. ANIGUSE. Athubutu” – ZITTO

Related posts