#ChukiNjeNje: Rapa 50 Cents Afafanua kuhusu “Bifu” lililopo Baina Yake na Mtoto wake Mkubwa !!

RAPA Jackson “50 Cents” Curtis ambaye pia ni Hit Maker wa Track ya “In Da Club”, amethibitisha namna ambavyo hampendi tena Mtoto wake Mkubwa, Marquise Jackson kama ilivyokuwa mwanzo.

Akizungumza kupitia Instagram Live, 50 Cents amekiri kutokuwepo na maelewano mazuri na mtoto wake huyo kwa muda mrefu sasa, huku akitoa lawama kubwa kwa mzazi mwenzake ambaye ni mama mzazi wa Kijana wao kuwa yeye ndiye chanzo cha “sumu” kubwa iliyoko baina yao wawili.

50 Cents ambaye hivi majuzi ameachia kitabu chake chenye jina la “Hustle Harder, Hustle Smarter” amekiri kabisa kuwa ni jambo la kuhuzunisha na kusikitisha kufikia hatua hiyo ambayo hakluitarajia hata kidogo, lakini hakuna namna, ni lazima mambo yaende sababu Marquise ni Mtu mzima kwa hivi sasa.

“Unapokuwa unaomba Mungu upate Mafanikio, huwa unaombea hata kile kitakachokuja ndani ya Mafanikio hayo. Mwanangu alipata kila kitu alichohitaji na ilinilazimu mpaka kutoa Dola Milioni moja kwa ajili ya Mahitaji katika Malezi yake”

KWA Mujibu Wa Baba Yake, Marquise baada ya kusitishiwa Huduma, alifikia Hatua ya Kuuza Vito vya Thamani

Katika Hatua Nyingine, 50 Cents amedai kuwa hakuwahi kuhisi kama Mafanikio yake yangemgharimu mtoto wake wa kwanza kabisa, ambaye alimpenda kwa dhati, huku lawama kubwa zikiwa ni kwa mama yake na Marquise

Alipoulizwa kuhusu kupuuzia tabia za mtoto wake na kuzichukulia kama ni sehemu ya ujinga, 50 Cents alisema hata siku moja hawezi kwa sababu yule ni mtu mzima tayari

“Marquise hivi sasa sio mtoto mdogo… Miaka 24 sio Umri mdogo. Ni mtu mzima mwenye maamuzi yake. Kipindi kile enzi zetu, marafiki zangu wengi katika mitaa yetu walikuwa wakipata watoto wakiwa na Umri wa Miaka 15, sasa yeye ana miaka 24”

50 CENTS anadai kuwa, Mzazi Mwenzake ambaye ni mama wa Marquise, ndiye amekuwa chanzo cha Sumu iliyopo baina yake na Mtoto wake huyo wa Kwanza

Aidha 50 Cents amemalizia kwa kudai kuwa, ilifikia hatua kijana wake huyo kuanza kuuza vito vyake vya thamani baadah ya 50 Cents mwenyewe kusitisha kumpatia pesa ya matumizi

Related posts