JAGUAR : ” Utaratibu Wa Chakula Kila Wiki Bado Unaendelea” (PICHA)

MBUNGE wa Jimbo la Starehe Nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi maarufu kama Jaguar, amesema kuwa utaratibu wa kutoa Chakula kwa Watu wasiojiweza katika Kipindi Hiki cha kujikinga na Maambukizi ya Virusi Vya Corona, bado unaendelea kama ulivyo katika maeneo mengine.

Kupitia Ukurasa Wake wa Facebook, Jaguar ambaye ni msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Kenya, aliandika kuwa utaratibu wa kugawa Chakula kila Wiki kw Wananchi wanaosumbuliwa na Magonjwa mbali mbali, Walemavu (PWDs) sambamba na Wazee wasiojiweza bado utaendelea mpaka pale Tatizo la Corona litakapopungua.

Jaguar na Timu yake wamekuwa wakipita katika maeneo mbali mbali kutoa msaada wa Vyakula na baadhi ya Vifaa vya kujikinga na Corona katika Jiji la Nairobi, huku wakiwasihi wananchi hao kuchukua tahadhari kubwa sana na kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya ili kuhakikisha wanatokomeza Maambukizi ya Virusi vya Corona

Pia Jaguar amesisitiza na kushauri mammlaka husika kutumia utaratibu maalum kuhakikisha wanawasaidi wananchi wa Kenya wanakuwa katika utulivu na amani.

Related posts