#Corona : Salon Hazitofunguliwa Nchini Uingereza

KATIBU wa mambo ya Nje Nchini Uingereza, Dominic Raab amesema kuwa Salon zinazoshughulika na Masuala ya Urembo na Nywele hazitofunguliwa mpaka itakapofika Julai 04.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson kutamka kuwa kutakuwa na awamu takriban Tatu za kuanza kuruhus wananchi wake kuanza kurejea katika majukumu ya Kila siku na kupounguza makali ya “Karantini”

Pia katika Hotuba yake, Waziri Mkuu aliagiza kuanza kuzirejesha Huduma mbali mbali mnamo mwezi Julai ambazo hufanyika Nchini humo ili kuepukana na changamoto mbali mbali za Kiuchumi kwa Wananchi wa Uingereza.

Hata Hivyo, Dominic aliongeza kuwa kutokana na tamko la waziri Mkuu kuzirejesha Huduma mbali mbali, Kuna baadhi ya Huduma ambazo bado zitabaki zimefungwa mpaka Itakapofika Julai 4, ili kuepusha msongamano wa watu na kusambaa kwa Maambukizi ya Virusi Vya Korona. Huduma hizo ni Pamoja na Salon, Migahawa, Bar na Pub zilizoko mitaani.

Related posts