EMINEM: “Huwa Nina-Google Mashairi Yangu”

RAPA Eminem a.k.a Slim Shaddy ni mmoja kati ya Wasanii wakongwe na wenye Heshima kubwa sana katika Muziki wa HIP HOP Ulimwenguni kote, ni hiyo ni kwa sababu ya Ubora wa Nyimbo zake na mashairi yenye “Ubabe” wa kutosha katika Soko la Muziki.

Lakini kama hukuwahi kufahamu, Eminem ni msanii ambaye anakiri kuwa ameshafanya Nyimbo nyingi sana mpaka huwa inamlazimu ku-google Mashairi yake ili asije akafanya makosa ya kurudia mashairi ambayo amekwisha wahi kuyaandika katika nyimbo zake zilizopita.

Eminem ambaye kwa hivi sasa anasumbua na Kwaju la “Godzilla” ameongeza kuwa, ameshaimba kuhusu matukio mbali mbali na mengi sana, na ameshafanya kazi nyingi sana, na kuna muda huwa anahisi hakuna kitu kigeni ambacho hajakifanyia kazi ama kukitungi mashairi.

” Ukiwa umeshatengeneza Nyimbo nyingi sana kuhusu kila kitu, huwa inachanganya sana kiasi fulani. Huwa inafikia muda hata unagusia kitu ambacho tayari ulishawahi kukizungumzia. Kuna Muda huwa inanilazimu tu nipitie Google kujua kama nimeshawahi kuzungumzia Jambo ili nisije nikalirudia kabisa.” Alisema Eminem

Related posts