MFUGAJI ALIYEOZESHA WATOTO ILI KULIPA FIDIA YA NG’OMBE AOMBA KUONANA NA RAIS MAGUFULI


Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa wilaya ya kiteto mkoani manyara ameomba kuonana na Rais Magufuli ili aweze kumsaidia kupata Ng’ombe zake zaidi ya mia tatu zilizokamatwa kimakosa kwa madai ya kukutwa kwenye hifadhi
James Satoro ametoa ombi hilo kwa Rais John Magufuli kupitia vyombo vya habari baada ya kudai kukamatwa kwa ng’ombe zake ambao waliingia katika mbuga ya kuishilbo mkoani humo tarehe tano mwezi wa tano mwaka huu 2020
Anadai baada ya kutokea kwa tukio hilo amekuwa akifuatilia kwa ukaribu bila mafanikio baada ya kutolewa uamuzi wa kurejeshewa ng’ombe hizo na mahakama ya rufaa ya mkoa wa dodoma
Kutokana na hali hiyo imepelekea kukimbiwa na wake zake sita na kuamua kuwaozesha watoto wake wa kike ambao wanaumri mdogo ili arudishe fidia kwenye ng’ombe zake

Related posts