KIKONGWE mwenye Miaka 108 Hatimaye amepona Maambukizi ya Corona : “Nilipangiwa Kupona”

SYLVIA GOLDSHOLL alifanikiwa kukwepa Mishale Mingi hatarishi ikiwema “Mafua ya Hispania (Spanish Flu) ya Mwka 1918, Vita Kubwa Mbili za Dunia, Anguko la Kiuchumi Duniani na safari Hii amefanikiwa Kupona kabisa Maambukizi Ya Virusi vya Corona.

Mwanamke huyo mwenye Umri wa Miaka 108 kutokea New Jersey Nchini Marekani, hivi sasa ni mwenye tabasamu mwanana akiwa na afya yake njema kabisa baada ya kuwa ni mmoja kati ya “Kikongwe zaidi” aliyepona maambukizi ya COVID 19

Bi. Goldsholl aliingia katika Historia ya kuwa na furaha zaidi mnbamo April 15 Baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali ambako alikaa kwa Takribani Siku tisa baada ya kubainika kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni hatari zaidi kwa Watu wenye Umri kama wa Kwake.

Naye Binamu wa Bi. Godsholl, Nancy Chazen, anadai kuwa, baada ya kupewa taarifa kuwa Ndugu yao alikuwa na maambukizi hayo, alihisi na kuamini kabisa huo ndo ulikuwa Mwisho wake katika safari ya maisha Yake hapa Duniani.

“Baada ya kupewa Taarifa kuwa alikbainika kuwa na maambukizi hayo, tuliamini hatutomuona Tena kutokana na Umri wake. Ninakumbuka nilipopigiwa Simu kuwa Amepona, kila mtu alishangaa na kuwa na mshtuko wenye Furaha kubwa sana. Mungu ni mwema” Alisema Nancy

Kwa Upande Wake Bi. Goldsholl baada ya kuulizwa namna ambavyo anajisikia baada ya kupona COVID 19, alisema kuwa amepona kwa sababu Mungu alimuumba ili apone na kuishi.

“Nimevuka matatizo Yote Makubwa na hatari kwa sababu nimepangiwa Kuishi na kupona katika Misuko suko yote”

Goldsholl aaliadhimisha Siku Yake Ya Kuzaliwa Mnamo Disemba 29,2019 ambapo alitimiza Miaka 108, huku sherehe yake ikihudhuriwa na Meya wa Eneo la ALLENDALE, New Jersey Marekani

Related posts