#KumekuchaMitandaoni: Hivi Ndivyo Ilivyo Mitandaoni Baada ya Rais Magufuli Kuruhusu Michezo Kurejea !

KATIKA Furaha ambayo wanayo watanzania Wengi hasa wadau wa Michezo na Mashabiki, ni baada ya siku ya Leo ambapo Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli kuagiza Mamlaka Husika na Masuala ya Michezo kuarejesha Ligi mbali mbali za Michezo sambamba na michezo Mingine kuanzia Juni 1.

Kauli hiyo imetolewa Mapema Leo wakati rais magufuli alipokuwa akiapisha Viongozi Walioteliwa, Katika Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma, sambamba na kuruhusu Vyuo vikuu na Kidato cha Sita kurejea katika Masomo yao.

Sasa, kunako Mitandao mbali mbali ya Kijamii, Wadau mbali mbali, Viongozi Vilabu mbali mbali vya Kimichezo, na mashabiki mbali mbali, wameonesha namna ambavyo wameipokea Kauli hiyo ya Serikali kwa njia tofauti tofauti.

  1. KLABU YA YANGA SC

Kupitia Ukurasa wao Wa Instagram mapema Hii Leo, Klabu ya Yanga wao wamepost Kauli ya Rais Magufuli wakati akiruhusu kurejeshwa Rasmi kwa Michuano Ya Ligi zote ambazo zilikuwa zimesimamishwa ili kupisha Maambukizi ya Corona

β€œKatika trend tuliyoiona sina uhakika kama kuna mwanamichezo aliyekufa kwa corona na michezo ipo mingi kila mmoja ana michezo yake, lakini michezo inasaidia kupambana, kwahiyo kuanzia Juni 01,2020 michezo irudi kama kawaida, ligi mbalimbali” -Rais Dkt. John Pombe Magufuli.”

2- HAJI S. MANARA

Kwa Upande Wa Instagram Account ya Msemaji wa Klabu ya “Wekundu Wa Msimbazi”-SIMBA SC, Haji S. Manara naye kwa upande wake aliipokea taarifa hiyo kwa Style ya aina yake huku akionesha kurusha Dongo kwa Wapinzani wao wa Jadi

“Majuzi nilisema anaenuna mm kumsifu Rais wa nchi anitumie zile picha nilizowaomba, aweke DM na CV yake.
Juni Mosi kwani lini? Kwa hyo ndio kusema De la Boss anakuwa Msemaji aliyeshinda medali nyingi zaid Tanzania πŸ€ͺ?
Kama nawaona Utopolo jinsi walivyovimba πŸ€ͺ Mnuno kama wote vile πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜…πŸ€£πŸ˜…”

4- MHE. MWIGULU NCHEMBA

Kwa Upande Wake Dk. Mwigulu Nchemba kupitia Instagram Account Yake, yeye hakusita kutoa “Big Up” kwa Rais Magufuli kwa Kuandika Haya:

“Proud of you my President. Mwanzoni wachache na kwa udogo wao walibeza, Siku hizi Dunia nzima wanakaa kwenye TV wakisikia unahutubia Ili wachangamkie mwelekeo unautoa. Hawataki kubaki nyuma Wala kupotea njia.. Hii inaitwa Taifa Dogo litashinda Taifa Kubwa. Big up My President”

4- KLABU YA SIMBA SC

Kwa Upande wa Instagram ya Wekundu wa Msimbazi-SIMBA SC wao kama kawaida walitupia Dongo kwa Wapinzani wao wa Jadi, Yanga SC kwa kandika Hivi:

“Wanasimba baada ya Rais Magufuli kuruhusu michezo ikiwepo Ligi Kuu kuanzia Juni 1, 2020 πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
.
Wapinzani 😌😌😌 #NguvuMoja:

Related posts