SWIZZ BEATZ: “Wasanii wa Sasa Wa Hip Hop wanatakiwa Kulipa Kodi kwa Waliofungua Njia”

Muandaaji wa Muziki wa Hip Hop Nchini Marekani, Kasseem Dean “Swizz Beatz” anaamini huu ni muda muafaka kwa Wasanii mbali mbali wa Hip Hop Nchini Marekani na hata ulimwenguni kote, kuanza kurudisha Matunda na fadhila kwa Wakongwe wa Muziki huo ambao wameufikisha Hapa Ulipo hivi sasa

Swizz ambaye pia no mmoja kati ya Rappers wenye balaa kubwa kila wanapoachia “mikwaju” yao, aliyasema hayo kupitia Instagram Live alipokuwa akizungumza na Mkongwe mwenzake kwenye soko la Hip Hop, Joe Budden.

Swizz Beatz na Mke Wakje Alicia Keys

Hit Maker huyo wa “Money In The Bank” ameongeza kuwa huu ni muda muafaka kwa Wasanii hao wa Hip hop kuanza kulipa Kodi zao kwa Waanzilishi wa aina ya hii ya Muziki maana ni kama hakuna wanachojivunia kutokana na harakati zao za kuahakikisha kuwa muziki wa Hip Hop unapata heshima kubwa ulimwenguni

“Ninataka kuchangisha Mamilioni ya Dola kwa kila Mtu ambaye ni nembo iliyoanzisha muziki wa Hip Hop, Dj Kool Herc na wengineo wote. Ukwli ni kwamba hivi sasa hatutoi Kodi kwa watu hao ambao walianzisha matamasha ya Hip Hop” alisema Swizz Beatz

Pia Swizz alitaja baadhi ya Waanzilishi hao ambao walipambana kufa na kupona na kuusimamisha Muziki wa Hip Hop, akiwemo Melle Mel, Grandmaster Flash, Sugar Hill Gang na wengineo kuwa wanahitaji japo Kiashi cha USD Milioni moja kwa namna ambavyo wametufikisha hapa tulipo

“Tunahitaji kuanza kwa Wabunifu hawa sehemu ya mapato yetu ili kuwapatia japo chakula Familia zao. Hawa ndio waliotupatia Uhuru wa Kuongea na kupiga hatua zaidi kupitia muziki wa Hip Hop”… Alisema Swizz Beatz

Related posts