#MtotoWaKishua: Rick Ross Amnunulia Binti Yake Gari Hili La Kifahari Masomo Yake.

UKITIZAMA Kwenye Instagram Story ya Rapa Kutokea Nchini Marekani, William Leonard Roberts II maarufu kama “Rick Ross”, utakutana na Video Clip ambayo inaonesha Zawadi kwa Binti yake wa Kike anayeitwa Toie Roberts (18) ikiwasilishwa Nyumbani kwake, huku akitamka kuwa hiiyo ndiyo tafsiri halisi ya Utajiri na Sura ya Utajiri kwa wale wasioelewa tafsiri ya Utajiri.

Rozay ambaye alizaliwa Januari 28,1976 aliamua kumnunulia Binti yake Huyo Gari la kifahari aina ya MERCEDES BENZ G CLASS 2020 maarufu kama G Wagon g63 2020 baada ya kuhitimu masomo yake ya High School na kutunukiwa “Diploma”

Kupitia kipande hicho cha Video, Hit Maker huyo wa “Aston Martin Music” alioneakana akiwa anarekodi wakati Gari hiyo inasogezwa mbele yake, huku akiwaomba watu ambao wanamfuata Binti yake huyo kwenye ukurasa wake binafsi wa Instagram, wamjulishe kwa “kumtag” ili aone zawadi yake na pongezi moja kubwa ya gari hilo la Kifahari linalogharimu zaidi ya USD Milioni Moja.

Kwa Upande wa Toie ambaye hiv majuzi tu ametimiza Umri wa miaka 18, naye alipost Kipande cha Video kinachoonesha “chuma” hicho kikishushwa nyumbani klwa baba yake huku akionesha kufurahishwa na Gari hilo la kifahari Lenye Rangi Ya Blue.

Gari aina ya Mercedes Benz-G Wagon 2020 (G63) alilonunuliwa Toie Na baba yake Rick Ross

Tofauti na Tukio Hilo, Mwaka 2018, Rick Ross alimnunulia tena Binti yake Toie Gari la Kifahari aina ya Bentley, baada ya kutimiza umri wa Miaka 16 yaani “Sweet 16” na kuzua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii na vyombo mbali mbali vya habari.

Related posts