UJUMBE WA AUNTY EZEKIEL KWA BINTI YAKE: “Naomba Kwa Hapa tulipofikia Mwanangu, Utanisamehe……. “

BINTI wa Kike wa Muigizaji wa Filamu hapa nchini Tanzania (Bongo Movie), Aunty Ezekiel, ambaye anaitwa “Cookie” hatimaye amepiga hatua nyingine katika maisha yake hasa kwa kuongeza Umri mwingine, akiwa mwenye afya nzuri na tabasamu Mwanana.

Hiyo imethibitishwa kupitia instagram account ya Mama yake (aunty Ezekiel) ambaye aliandka ujumbe mrefu ulikuwa na maelezo ambayo kila mtu amebaki na uelewa wake katika tafsir yake kulingana na namna ambvyo Aunty mwenyewe aliandika ujumbe huo na kusomwa na maelfu ya Wafuasi wake

Katika Ujumbe huo, Aunty ameelezea namna ambavyo amejitoa vilivyo kuhakikisha Cookie anapata malezi na mahitaji sahihi katika wakati muafaka, ili kuendelea kumfanya awe mtoto imara, bora na mwenye heshima kwa kila mtu, kitu ambacho kuna baadhi ya wazazi hufanikiwa na hata wengine kushindwa.

Ukiusoma kwa umakini zaidi ujumbe huo, utabaini kuwa Aunty Ezekiel ameweka bayana kuwa alihakikisha Cookie anakuja duniani na kuwa mtoto bora ikiwa ni kuifanya nafsi ya Baba Yake (Mose Iyobo) ifurahie zaidi licha ya kukutana na changamoto mbali mbali kama vile Matusi, Fedheha, Lawama na hata kupigana ili furaha yake isiende mbali

Aunty aliandika Hivi:

“Happy Bday Roho yangu……
Inshallah Nakuombea Maisha marefu yenye Amani na Baraka tele mbele yake kwani naamini watoto wote wanakuwa kwa Rehma zake Mwenyezi Mungu na sio Mtu mwingine I try my Best kukupa Furaha ktk Maisha yako na Furaha ya kwanza ktk Maisha yako Naamini ni Baba yako kabla hata yangu mm hvyo bac nikaamua kuingia lawama,Fedheha,Matusi hata kupigana kuhakikisha tuu Furaha yako haiendi Mbali ila tuu Naomba kwa hapa tulipofika Mwanangu utanisamehe na Naomba nikuanzishie Maisha Mapya ambayo Naamini unaweza usifurahie ila utakuwa Sawa siku moja….na Maisha yataendelea kwakuwa ni Mtoto wa kike hata kama sio leo ila ipo siku utaelewa Mamang furaha yako ni Bora ila yangu pia ni bora maradufu…..unaambiwa tetea Nafsi yako kabla ya Mwenzako mm nikajifanya tetea yako kwanza kabla yang NIMESHINDWA MM AM SO SORRY MY BABY 🙏😥
HAPPY BDAY ONCE AGAIN HONEY
@cookielaprincess
@cookielaprincess
#cookieshez5💞🍬💥
#Mybdaygirl❤
#2020❤

INGAWA kuna baadhi ya “Waungwana” wametengeneza Tafsiri ya Ujumbe huo kuwa huenda Aunty Ezekiel anataka kufanya mabadiliko ya Malezi kwa Binti yao huyo kutokana na Umri kusogea hasa kwa kutokumuweka zaidi kwenye “Spotlight” na masuala ya kimitandao na malezi kiujumla, kuna baadhi wanaamini kuwa huenda Muigizaji huyo akawa ameachana rasmi na Mose Iyobo na sasa yuko tayari kuanza kumlea mtoto wake katika misingi yake yeye kama yeye.

Licha ya Yote, Tunamtakia Maisha Marefu Mtoto Cookie !!!. Happy Birthday !!!

Related posts