DJ KHALED: “Rihanna Aliponigusa Mara Ya Kwanza Begani, Nilihisi Kuchanganyikiwa”

SIO Mara ya Kwanza kusikia na Hata kuwaona Mastaa wakubwa Duniani kote wakikiri kuhisi “kupagawa” pale wanapoguswa ama kukutana na Mastaa wenzao ambao wamekuwa wakliwafuatilia mara kwa mara katika maisha yao.

Hii Pia iliwahi kuthibitishwa na Rapa kutokea Nchini Marekani, Chance The Rapper, ambaye alijikuta akihisi kuchanganyikiwa baada ya Beyonce kumpa Busu wakati Rapper huyo akifanyiwa Mahojiano katika moja ya Tamasha Nchini Humo.

Safari Hii, Dj Khaled amekiri wazi kuwa alihisi kurukwa na akili baada ya Rihanna kumgusa katika bega lake kwa mara ya kwanza, na hiyo ni kwa sababu hitmaker huyo wa “Wild Thoughts” huwa anampenda sana Bibie Huyo.

Robin “Rihanna” Fenty

Dj Khaled alitoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza kupitia Instagram Live na producer mkongwe Duniani, Timberland, ambapo alimuambia kwamba, alihisi kuchanganyikiwa kabisa baada ya bibie Rihanna kumgusa Begani na kumwambia kuwa “Suti” aliyokuwa ameivaa ni Nzuri sana na imempendeza Dj Khaled.

“Wacha nikuambie Kitu Timb (Timberland). Pale Rihanna anapojitokeza sehemu, huwa ni Balaa… Kila sehemu Riri (Rihanna) akijitokeza, huwa ni balaa tupu. Ngoja nikuambie Hadithi moja. Rihanna aligusa Suti yangu siku moja na kuniambia ina muonekano mzuri. Akili nilihisi imeniruka” alisema Khaled.

Pia katika jambo Lingine, Dj Khaled ambaye pia ni Producer Mwenye sifa kubwa Duniani, amesema anajivunia sana kufanya kazi na Rihanna.

“Bado Siamini kama Nimefanya Kazi na Rihanna kwenye wimbo wangu wa WILD THOUGHTSaliongeza Dj Khaled

Related posts