FBI YAINGILIA KATI TUKIO LA MTU MWEUSI ALIYEUAWA NA ASKARI WA KIZUNGU KWA KUMKANDAMIZA NA GOTI SHINGONI.

Shirika la upelelezi la nchini Marekani la FBI limeanza kufanya chunguzi juu ya tukio la raia mweusi wa marekani ambaye ameuawa na polisi wenye asili ya kizungu kwa kumkandamiza kwa goti shingoni.

Licha ya raia huyo George Lloyd kuwaomba askari hao wasimkanamize kwakuwa anashindwa kupumua bado askari waliendelea kumkandamiza hadi kifo chake mnamo 25 Mei 2020.

Kupitia video inayowaonesha askari hao wakifanya kitendo hicho raia wa nchi tofauti wakiwemo wamarekani wenyewe wameonesha kutofurahishwa na kitendo hicho kiasi cha baadhi yao kuanza kurusha mawe katika magari ya polisi hasa katika eneo la Mineapolis kulipotokea mkasa huo.

Kuna taarifa kuwa askari waliohusika na tukio hilo wamesimamishwa kazi na tayari hatua zaidi za kiheria zinaendelea dhidi yao.

“Siwezi kupumua,” alisema kwa kurudia lakini polisi hawakusikiliza.

Aliyeshuhudia tukio hilo alimwambia afisa wa polisi aliyekuwa amemkandamiza kwa kumueleza kuwa damu zinamtoka puani lakini askari huyo hakuonesha kujali.

Related posts