#Mnazingua: MEGHAN THEE STALLION Hajapenda hili kutoka kwa Wamiliki wa Instagram !!

KIUHALISIA Sio kila mtu huwa anapenda Mabadiliko ama maboresho ya aina tofauti katika “App” mbali mbali hasa za mitandao ya Kijamii. Lakini pia, sio kila mtu huwa anachukia maboresho ya “app” hizo za mitandao ya kijamii.

Meghan Thee Stallion, ni mmoja kati Ya watu wachache ambao pengine hawajafurahishwa na mabadiliko mapya katika “account” yake ya Instagram na kuamua kuwapa “makavu” wamiliki na hata mafundi wanaoshughulikia mabadiliko katika mtandao huo.

Rapa huyo wa kike ambaye hivi sasa anafanya Vema na mkwaju wa “Savage Remix” aliomshirikisha bibie Beyonce, amechukizwa haswa na mamboresho mapya katika account yake hiyo na kuamua kuliweka wazi jambo hilo huku akiwasihi wamiliki wa mtandao huo kumrudishia muonekano wa account yake uliokuwepo kabla.

Pengine unaweza kuhisi labda muonekano mpya umemshinda bibie huyo hasa katika matumizi yake, lakini Meghan amesisitiza kuwa yeye huwa hapendi maboresho mapya pasipo kuwa na taarifa angalu.

Pia Meghan Thee Stallion ameongeza kwa, kama wamiliki wa app hizo wanapenda kuboresha App zao, kwanini wasianzishe App nyingine ambazo angalau zingeashiria kuwa kuna kitu kipya, ili kama kuna watu watapenda app zenye maboresho mapya basi watumie hizo, kuliko kuboresha tu kiholela na kusababisha Usumbufu

Katika Kukazia zaidi, Meghan Thee Stallion ameomba Instagram wamrudishie muonekano wa zamani katika account yake hiyo.

Related posts