KINGWENDU: “Mwanza Vijijini Kumesababisha Tusifanye Filamu za Vichekesho”

KAMA utakuwa unakumbuka vizuri sana, kipindi cha Nyuma Filamu nyingi sana za Vichekesho zilikuwa ni sehemu ya Gumzo na hata kufikia hatu kupendwa sana na wadau wengi sana wa tasnia hiyo hapa Nchini Tanzania.

Katika filamu hizo, ulikuwa unakutana na muunganiko wa wasanii wengi sana wa vichekesho, hali ambayo iliashiria kuwa huenda umoja wao ukaendelea kutpatia burudani na wao kupata matunda kutokana na kuwepo kwa mauzo mengi mitaani.

KINGWENDU ni miongoni mwa wachekeshaji wakongwe ambao pia walionekana sana katika Filamu hizo za vichekesho na kuleta ladha nzuri sana huku akishirikiana na wenzake kama vile Pembe, Bambo, Senga, Muhogo Mchungu, Marehemu King Majuto, na wengineo kadha wa kadha.

Katika kufafanua kupungua kwa filamu hizo sokoni, Kingwendu amedai kuwa hivi sasa wasanii wengi wa Vichekesho wana majukumu mengi sana ya kifamilia na muhimu kutafuta pesa ili kuhakikisha familia zao zinajikimu hasa katika mahitaji ya kila siku. Hivyo kwa hivi sasa wasanii wengi wa vichekesho wamekuwa wakikimbilia katika mikoa mingine nje ya Dar Es Salaam kutafuta pesa kupitia maonesho mbali mbali ya vichekesho.

Pia Kingwendu kwa upande wake, ameongeza kuwa hata ule ushirikiano wa kuachia filamu nyingi za Vituko na wakongwe wenzake, umepungua kutokana na yeye kuwa “Bize” na matamasha yake katika maeneo ya Mwanza Vijijini ambako hutumia mpaka takribani Miezi nane pasipo kurudi Dar Es Salaam akitafuta pesa.

“Wakazi Wengi wa dar Es Salaam wamekuwa Busy na mambo yao mengine. Hivyo inatulazimu kuenda Mikoani ili kufanya maonesho yetu, maana hata ukisema uandae matamasha ya aina hiyo Jijini Dar Es Salaam mara nying huwa ni ngumu kwa sababu tunaishi nao, na wametuzoea. Kwa hiyo ni ngumu kuandaa tamasha na watu wakajaa kama inavyokuwa Mikoani. Mimi huwa natumia mpaka Miezi Nane nikizunguka Mwanza Vijijini kutafuta Pesa kupitia matamasha ya vichekesho. Kukutana na wenzangu inakuwa ni ngumu ili kuandaa Filamu.” alisema Kingwendu

Related posts