LUDACRIS: “Niliongea na Familia Ya George Floyd”

RAPA Ludacris ni Miongoni mwa watu maarufu ambao waliungana na Familia ya Marehemu George Floyd Nchini Marekani, katika Msiba sambamba na Mazishi, ikiwa ni sehemu ya kuguswa na kitendo cha “kikatili” kilichofanywa na Baadhi ya Askari Polisi ambao walipelekea Kifo cha Mmarekani mweusi huyo.

Ukiachilia mbali kuhusika ama kujumuika na Familia ya marehemu, Ludacris pia aliungana na maelfu ya raia wa Marekani ambao walikuwa katika maandamano ya kupiga vita Ubaguzi wa rangi ambao umekuwa ukisababisha vifo vya “wamarekani Weusi” na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo George Floyd ambaye alipoteza maisha May 25,2020 huko Minneapolis, Nchini Marekani.

Licha ya kuhusika katika hatua zote hizo. Ludacris anakiri kuwa alipojumuika na Familia ya Marehemu Floyd, alipata nafasi ya kuzungumza nao kiundani na kuna mambo mengi sana ambayo waliyazungumzia ingawa kwa upande wake hawezi kuyafafanua hadharani kwa sababu ni mambo ya Siri.

LUDACRIS: Yuko tayari kushirikiana na watu wengine kuhakikisha familia ya Marehemu George Floyd inasikilizwa vema. (Picha: Ludacris Instagram)

Hit Maker huyo wa “My Chick Is Bad” ameongeza kuwa, Familia hiyo ya Marehemu kiuhalisia inatakiwa kusikilizwa na mamlaka husika hasa serikali ya Nchini Marekani, kutokana na namna ambavyo wameumizwa na kifo cha Ndugu yao na kupelekea maandamano makubwa ya kupinga Ubaguzi wa Rangi na kuhitaji haki ya msingi kwa Marehemu George Floyd.

Pia Ludacris ambaye jina lake halisi ni Christopher Brian Bridges ameongeza kuwa, Familia ya Marehemu Floyd ina mengi ya kuzungumza ingawa hivi sasa wapo katika Kipindi kigumu sana, lakini bado wana nguvu, ni imara na wana ujasiri na ameahidi kuhakikisha anashirikiana na Watu wengine kufanikisha mahitaji yaliyozungumzwa

Related posts