JIDE JAY DEE: “Nawasihi Msiwe mnaniletea Kolabo Za Mapenzi… Joh Makini Alitetemeka !!”

SIO Mara ya kwanza kusikia kwamba kilichopo nyuma ya kazi nzuri sana ambazo tumekuwa tukizifuatilia, kuzipenda na hata kuzipongeza hasa kutoka kwa Wasanii mbali mbali ulimwenguni, huwa kuna matukio mengi sana ambayo hatuyafahamu na hata tukiyafahamu , basi huwa tunashangaa sana na pengine kubaki tukicheka ama kubaki vinywa Wazi.

Ndani ya Wiki Hii, Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya hapa Nchini Tanzania, Judith Wambura maarufu kama “Lady Jay Dee” alikuwa akiadhimisha Siku yake ya Kuzaliwa na alionekana kuwa ni mtu mwenye furaha kubwa sana baada ya kupiga hatua katika umri na maisha yake kiujumla.

Kupitia furaha aliyokuwa nayo, Jide alizungumzia tukio ambalo lilijitokeza wakati wakifanya Kazi ya Kurekodi Video ya “Kiwembe” ambayo ameshirikishwa na Rapa Joh Makini kutokea katika Familia ya Weusi, ambayo mashabiki wengi sana wanaisubiri kwa hamu.

Katika maelezo yake kupitia Instagram account yake, Jide aameandika kwamba wakati wanafanya Video hiyo, Joh Makini alitakiwa kuigiza kama Boyfriend Wake na kitu ambacho kilijitokeza, Joh Makini alianza kutetemeka hadi akaanguka.

Kutokana na tukio hilo, Jide amewasihi wasanii mbali mbali wasiwe wanamletea Kolabo za mapenzi maana kumtizama machoni tu hawawezi, ingawa anahisi ni kwa sababu wanamuheshimu sana ndio maana wanatetemeka

Naomba Tumnukuu Hapa tafadhari:

“Ngoja niwapeni sasa story ya @johmakinitz
Tukiwa tuna shoot Kiwembe ilibidi a act kama boyfriend wa Komando. Huwezi amini alitetemeka hadi akaanguka. Ninachoshukuru @juma_jux alirekodi hako ka video siku akibisha tunaka post… Ila Jux nirushie basi whatsApp naahidi sitakavujisha 😂😂😂😂


Nawasihi msiwe mnaniletea Feat/Collabo za mapenzi maana kuniangalia machoni tu hamuwezi. Nimewahurumia sana

Lakini ni sababu mnamuheshimu dada mkubwa ndio maana mnatetemeka hata kunishika mkono tu. Ila mtetemeko wa Harmo nao ni kama wa Joh tu 😂😂
#Kiwembe
Hope y’all ready for it 👌🏾

Related posts