PROFESA JAY: “Tulianza na Mungu, Tumemaliza na Mungu”

JUMANNE ya Juni 16,2020, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli alivunja Bunge la Tanzania ili kuruhusu Wabunge kurejea katika Majimbo yao tayari kwa taratibu za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba 2020.

Katika hatua hiyo, wabunge mbali mbali kupitia vyama vyao na wao wenyewe binafsi walipata kwa nyakati na njia tofauti, walipata nafasi ya kuzungumza mengi kwa wapiga kura wao hasa kupitia vyombo vya habari na hata mitandao ya kijamii hasa kuwashukuru kwa kuwaamini mpaka kufikia hapo walipo hivi sasa

Mhe. Joseph Haule “Professor Jay” ambaye alikuwa akiwakilisha jimbo la Mikumi huko Mkoani Morogoro, kwa upande wake hakuona hiyana kuwashukuru wananchi wa Jimbo lake kupitia akaunti yake ya Instagram kwa kuwaambia kuwa Walianza na Mungu na hatimaye wamefanikiwa kumaliza na Mungu.

Tofauti na kushukuru Mungu, Pia Prof Jay ameweka wazi kuwa bado yupo na kupitia Tiketi ya chama chake, yaani Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo-CHADEMA, ametia Nia tena ya kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Mikumi.

Tunamnukuu :

“Tulianza na MUNGU Tumemaliza na MUNGU🙏🏻🙏🏻
Kwanza kabisa Namshukuru sana mwenyezi MUNGU kwa Baraka, Neema hii, kunilinda na kunipa Afya njema na Nguvu ya kuweza kutimiza yale ambayo wananchi wa Mikumi waliniamini na kunichagua nikawe muwakilishi wao Bungeni, Nawashukuru sana Wananchi wa jimbo la MIKUMI kwa ujumla wetu kwa kuniamini na kunituma kuiwakilisha MIKUMI yetu na Wilaya ya KILOSA Bungeni, Natumaini kwa kiasi kikubwa nimefanikiwa na nimeweza kutekeleza yale mliyonituma kuyasemea na kuyasimamia, NAWASHUKURU SANA, Nakishukuru sana chama changu DUME cha CHADEMA kwa kuniamini na kunipitisha kuwa mgombea kupeperusha bendera kwa tiketi ya Chama chetu pendwa kwenye uchaguzi wa 2015 na kuibuka kidedea pamoja na Misukosuko yote tuliyopitia lakini namshukuru Mungu ametuvusha Salama pongezi nyingi kwa JEMEDALI wetu @freemanmbowetz kwa kutuongoza vema na kwa weledi na ujasiri mkubwa Mwanzo Mwisho, shukrani kwa viongozi na wanachama wote wa ngazi zote wa CHADEMA kwa kuendelea kushirikiana na kushikamana na kuendeleza mapambano kama FAMILIA MOJA, NIPO, NILIKUWEPO NA NITAKUWEPO na nimetia NIA tena ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa JIMBO LA MIKUMI kupitia Chama changu cha CHADEMA Nawaomba sana wananchi wote wa jimbo la MIKUMI na wanachama wote Umoja na Ushirikiano zaidi na zaidi, Mwenyezi Mungu atubariki sote, KIPENGA KIMELIA, TUKUTANE FIELD🙏🏻🙏🏻”

Related posts