YOUNG DEE aanika Ukweli wake Kuhusu MR. BLUE

UKIACHILIA mbali ubora wake katika Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania “Bongo Flava”, Young Dee ni mmoja kati ya Rappers walioanza kupata umaarufu katika Umri mdogo na hata yeye anakiri hilo jambo. Mpaka hivi sasa, Young Dee “Paka Rapper” amezidi kusimama katika ubora wake ambao kila mtu ambaye anafuatilia muziki wa Bongo Fleva anafurahia kila kazi ambayo anaachia kwa mpangilio wake.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Hitmaker huyo wa mkwaju wa “Noma Kweli” ameweka bayana safari yake ya muziki ilipoanzia na kufikia hapo alipo, huku akiwataja na kuwashukuru watu ambao walikuwa nyuma ya safari yake na kufanikisha ndoto yake.

Katika maelezo yake, Young Dee ameweka wazi kuwa, Mr. Blue ndiye alikuwa sehemu ya safari yake ya kwanza kabisa ambaye alifungua njia ya kutimiza ndoto alizokuwa nazo katka tasnia ya muziki na hata kuufikia umaarufu na ukubwa ambao anao hivi sasa

Akiweka sawa maelezo yake kuhusu Mr. Blue ambaye amekuwa ni motisha kwa vijana wengi waliongia katika muziki wa Bongo Fleva, Young Dee amesema kuwa wakati anajifunza masuala ya muziki, ndoto yake ilikuwa ni kuwa kama Mr Blue kwa sababu kuna vitu alivyokuwa akivitamani kutoka kwake

MR. BLUE: Alifanikiwa kumpeleka Young Dee katika Studio za Dhahabu Records na kumkutanisha na Dully Sykes na Marehemu Pancho Latino, ikiwa ni baada ya kumtafutia studio nyingi pasipo na mafanikio yoyote. (Picha: Young Dee Instagram)

Tunamnukuu:

“Nilipokuwa najifunza kuimbaimba nikiwa mdogo sana, ndoto yangu ilikuwa kuwa kama @mrbluebyser1988! Nilikuwa natamani unyamwezi wake, style yake, mafanikio yake, alikuwa ndio kama kioo changu! Nilitamani siku moja walau nikutane nae nikiamini kwamba kukutana nae kungenifungulia mwanga wa sanaa yangu, kwani ningejifunza kuanza nikiwa mdogo kama alivyofanya yeye:

Mwaka 2003 nikiwa darasa la Tano, shule ya msingi Tabata Kimanga kipindi hicho nikiwa nachana chana tu darasani, washkaji zangu waliniambia kwamba Mr. Blue amehamia Tabata, na jioni hupenda kukaa sehemu flani karibia na shuleni kwetu, wakanisihi nifanye jitihada za kumtafuta Kwani atanisaidia kutoboa kimuziki.
Tulifanya jitihada mbali mbali, na siku moja tulifanikiwa kuonana na Blue, akiwa na kina Abby Skills. Nilichana mbele yake kwa aibu aibu, nikiwa na wasiwasi mkubwa kwasababu Blue alikua wamotoooo na bonge moja la bishoo, kuweza kupata ujasiri mbele yake ilikuwa changamoto kidogo.

Cha ajabu Blue aliona uwezo wangu pale pale, akanambia nifanye mazoezi zaidi kuweza kuboresha uwezo wangu. Kikubwa ambacho sitakaa nisahau kuhusu brother wangu huyu, ni namna alivyolichukulia swala lile kwa ukubwa, kwani aliniambia niende kwao Weekend iliyofatia, kuna CD ya beat nikafanyie mazoezi pale ajaribu kunirekebisha. Hamuwezi amini washkaji zangu, kitendo cha mimi mtoto wa kawaida kabisa kukubalika na Blue hadi kuingia nyumbani kwao Blue na kunisikilizisha beats, na kubond kama watu tuliokuwa tunajuana kitambo, ilinifundisha kitu kikubwa sana kuhusu thamani.

Long Story short, Blue aliweza kuniweka kwenye njia nzuri kimuziki. Safari yangu kimuziki ilianzia mikononi mwake. Alihangaika kutafuta maproducer wengi ili waweze kunirekodia nyimbo zangu bila mafanikio (ahadi zilikuwa nyingi), lakini hatimaye alinipeleka Dhahabu Record ambapo nilifanikiwa kurecord wimbo wangu wa kwanza kabisa katika maisha yangu, ambao ndio wimbo ulionitambulisha miongoni mwenu.

Brother Blue, kwa chochote nifanyacho leo, kilianzia kwenye hatua zile za Tabata, mchango wako kwenye sanaa yangu nitauthamini milele, bila wewe huenda ningepitia njia tofauti kufika hapa leo, na huenda isingekuwa nyepesi na yenye manufaa kama nilivyopitia kwako.”

Tofauti na Mr Blue, Young Dee a.k.a Young Dar Es Salaam amewataja watu wengine muhimu katika safari yake ya muziki akiwemo Dully Sykes pamoja na Marehemu Pancho Latino ambaye alikuwa ni mmoja kati ya Poducers wazuri sana hapa nchini Tanzania.

Related posts