Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza muda wakusitishwa kwa visa za bahati nasibu pamoja na zile za wafanyakazi wa kigeni hadi mwisho wa 2020

Wafanyikazi wenye ujuzi mkubwa wa kiufundi, wafanyikazi wasio katika sekta ya kilimo na maafisa wakuu wa makampuni wataathirika.

Ikulu ya Marekani imesema kwamba hatua hiyo itabuni ajira kwa Wamarekani wasio na kazi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Lakini wakosoaji wanasema kwamba Ikulu ya Whitehouse inatumia janga la corona ili kukaza sheria za uhamiaji.

Facebook Comments

Related posts