CPWAA:KUNA CHANGAMOTO KWENYE BONGO FLEVA HASA KWA WASANII WA KIKE

C Pwaa Ni Moja Ya Msanii Wa Muda Mrefu Katika Kiwanda Cha Muziki Nchini Tanzania Na Moja Kati Ya Msanii Ambaye Licha Ya Kuwa Anapotea Katika Muziki Kwa Kipindi Flani Lakini Anaporejea Mara Nyingi Huja Kwa Kasi Ya Ajabu Na Muitikio Mzuri.

C Pwaa Ambaye Kwa Hivi Sasa Anatarajia Kuachia Ep Yake Ikiwa Ni Miaka Sita Tangu Akae Kimya Katika Muziki ,Msanii Huyo Amezungumza Na Hitzone Ya Jembe Fm Na Kuweka Wazi Mengi Kuhusu Ujio Wake Katika Muziki Lakini Moja Na Kubwa Kuhusu Msanii Huyo Amezungumzia Nafasi Ya Wasanii Wa Kike Katika Muziki Wa Bongo Fleva Baada Ya Kuulizwa Wasanii Wa Kike Waliopo Ni Wangapi Wapo Katika Orodha Yake Na Amejibu Kuwa

“Kikweli Kuna Changamoto Kwenye Soko La Bongo Fleva Hasa Kwa Wasanii Wa Kike,Mimi Almost Wasanii Wengi Wa Kike Waliopo Nawakubali Na Nawapa Sapoti Na Hawako Wengi Sana Wanahitaji Sapoti Yetu Kwahiyo Nikisema Niwapange Kwenye List Haitakuwa Vizuri,Lakini Wasanii Wengi Wanafanya Vizuri  Kama Vanessa Mdee Amekuwa Akifanya Vizuri Na Juzi Hapa Nimesikia Taarifa Zake Namshauri Asikate Tamaa Yatapita Na Arudi Kwenye Mziki,Kuna Wasanii Wengi Sana ,Nandy ,Maua Sama Rosaree Na Bado Kuna Wakongwe Wanafanya Vizuri Kama Dada Jide,Grace Matata Na Wengine Wapya Kama Zuchu ,Frida Amani Kiufupi Wasanii Wa Kike Wote Nawasapoti Na Sina Daraja Kusema Nitamuweka Huyu A Huyu B.”

Amezungumza C Pwaa Na Kuongeza Kuwa Mashabiki Wategemee Uzinduzi Wa Ep Yake Hivi Karibuni.

Facebook Comments

Related posts