PREZZO:SIKUTAKA KUONEKANA KAMA SHABIKI NILIPOKUTANA NA JAY Z

Rapa Jackson Makini Kutoka Nchini Kenya Ni Moja Kati Ya Msanii Ambaye Amewahai Kukutana Na Rapa Kutoka Marekani Jay Z Akiwa Anawakilisha Afrika Ya Mashariki ,Prezzo Alikutana Na Jay Z Mwaka 2012 Akiwa Balozi Wa Kampeni Ya Watu Maarufu Iliyokuwa Na Dhumuni La Kupinga Umaskini Na Magonjwa Duniani.

Prezzo Alipata Nafasi Ya Kukutana Na Jay Z Licha Ya Kuwa Msanii Huyo Alikuwa Ni Shabiki Mkubwa Wa Jay Z Lakini Alipokutana Nae Hakutaka Kuonyesha Kuwa Ni Shabiki Bali Alitaka Kukaa Meza Moja Na Msanii Huyo.

Akizungumza Katika Mahojiano Na Chanzo Kimoja Cha Habari Nchini Kenya Prezzo Ameweka Wazi Hali Hiyo Na Kudai Kuwa

“Mimi Binafsi Sikutaka Kukutana Na Jay Z Kama Shabiki Yake Bali Nilitaka Kukutana Na Jay Z Kama Mtu Ambaye Ninataka Tukae Kuzungumza Na Nikafanikiwa Japo Ni Jambo Ambalo Linatokea Mara Chache Sana”

Amesema Prezzo Ambaye Pia Ni Moja Kati Ya Msanii Aliyeweza Kudumu Katika Heshima Ya Muziki Nchini Kenya.

Facebook Comments

Related posts