KCEE:NIGERIA BADO HATUNA MFUMO MZURI KATIKA MUZIKI WETU

Msanii Kcee Ambaye Pia Ni Moja Ya Mgurugenzi Wa Lebo Maarufu Nchini Nigeria Maarufu Kwa Jina La Five Star Music Ambayo Ilifanikiwa Kusaini Wasanii Akiwemo Harry Songs Pamoja Na Skibii Ambao Kwa Sasa Wasanii Hao Pia Wamejitoa Katika Lebo Hiyo Na Kila Mmoja Kuanzisha Safari Yake Kivyake.

Licha Ya Yote Hayo Kcee Bado Ameendelea Kufanya Kazi Na Akiwa Kama Msanii Ambaye Ana Uzoefu Wa Kumiliki Lebo Na Kusimamia Wasanii Ameeleza Moja Ya Changamoto Ambayo Bado Ni Kubwa Sana Katika Muziki  Wa Nigeria Katika Kusaini Wasanii Katika Lebo.

Kcee Amezungumza Hayo Akipiga Story Na Chanzo Cha Habari Cha Hip Tv Nchini Nigeria Na Kuweka Wazi Kuwa.

“Ninafikiri Ni Kitu Ambacho Ni Kigumu Hasa Katika Tasnia Yetu Hapa Kutokana Na Kukosa Mifumo Maalumu Ya Kuendesha Kazi Zetu Hivyo Imekuwa Ni Changamoto Ambayo Inapelekea Unakuta Msanii Anasainiwa Katika Lebo Lakini Anaishia Kufanyishwa Kazi Na Msimamizi Wake Kwa Madai Ya Kuwa Amewekeza Pesa Kwaajili Yake Na Hata Kwa Upande Wa Wasanii Akishasainiwa Anajisahau Na Anashindwa Kujiongoza Kwa Hiyo Mifumo Ni Muhimu Ili Kila Mtu Ajue Wajibu Wake Na Kila Mmoja Anufaike”

Amesema Kcee Ambaye Bado Anaendelea Kufanya Muziki Wake Pasipo Kujali Ama Kuwa Na Wasiwasi Juu Ya Lebo Yake.

Related posts