WAGOMBEA WA CCM UPANDE WA ZANZIBAR MSIUMIZANE

📻… “Niwaombe sana hasa wagombea wa CCM upande wa Zanzibar wawe waangalifu wasiumizane kwenye kunadi Sera zao maana kazi sio Urais tu. Hata kwenye Majimbo watia nia mtarogana bure na kuumizana bure atakayechaguliwa Mungu anamjua.”
.
.
“Tukigombana wakati wa kampeni tutapoteza Direction. Atakayechaguliwa wakati wa kampeni tumbebe na nafasi zipo nyingi za kuteua na hata sasa zipo kama Nne sijateua. Najiuliza nimteue nani? Muhimu ni tushike Dola kwanza.”

.
.
“Tanzania ina umuhimu kuliko sisi na niwathibitishie mambo yanaenda vizuri sana kila mahali mambo yanafanyika.” –
.
.

“Nchi hii ni tajiri. Nataka niwaambie ukweli ni tajiri kilichokuwa kinatusumbua ni ufisadi na wizi. Kilichokuwa kinapatikana kilikua hakiendi kwa walengwa. Kwani mimi ni Malaika? Ndege zimenunuliwa 11 mbona hazikununuliwa zamani?”
.
.
“Nimeambiwa Watia nia katika majimbo mengine wako zaidi ya 20. Mtaragona, mtaumizana bure. Atakayechaguliwa ni mmoja tu. Kuanzia kesho tarehe 1 mwenzi wa 7 ruksa WanaCCM kupita pita ofisini kuchukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania nafasi za uongozi.” –
.
.
Dkt. @MagufuliJP

Related posts