Maandamano dhidi ya vitendo viovu vya polisi yanaendelea nchini Marekani

Maandamano dhidi ya vitendo viovu vya polisi yanaendelea nchini Marekani katika miji ya Kenosha naPortland ambapo mtu mmoja aliuawa katika makabiliano kati ya waandamanaji wa vuguvugu la watetezi kwa mtu mweusi

Rais wa marekani anaendelea kuwataka raia kuheshimu sheria na amewashutumu maafisa wa miji hiyo kwa kuruhusu machafuko

Portland imekuwa kitovu cha maandamano dhidi ya ukatili unaotekelezwa na polisi na ubaguzi wa rangi tangu kutokea kwa mauaji ya George Floyd mmarekani mweusi huko Minneapolis mnamo mei 25 na kusababisha ghadhabu nchini humo na hata kimataifa

Trump anatarajia kuzuru mji wa Kenosha katika jimbo la Wisconcin Jumanne wiki hii

Aidha, Donald Trump ametoa rambi rambi zake kwa familia ya mtu aliyepigwa risasi na kuuawa huko Portland jumamosi wakati wa makabiliano kati ya wafuasi wake na waandamanaji kutoka vuguvugu la Black Lives Matter

Related posts