Polisi mkoani mbeya kusimamia Amani wakati wa kampeni za uchaguzi

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani mbeya Urich Matei amesema askari polisi ndani ya mkoa huo wako imara kusimamia amani wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu pamoja na uchaguzi wenyewe.

Akizungumza kwa njia ya simu Matei amesema kupitia Elimu ya usalama waliyoifanya ikiwamo kuyashirikisha makundi yote ya vijana pamoja na wazee ni maandalizi tosha ya kukabiliana na wale wote watakaojaribu kuvuruga amani ya ndani ya mkoa huo

Aidha kamanda Matei amewasisitiza wadau wote wauchaguzi kuzingatia sheria na miongozo yote ya uchaguzi kama inavyoelekeza ili kuepusha uwepo wa changamoto zisizo na ulazima wa kutokea

Related posts