Chama tawala Guinea chasema Conde atagombea muhula wa tatu

Chama tawala nchini Guinea kimethibitisha uvumi wa miezi mingi kuwa Rais Alpha Conde ambaye ana umri wa miaka 82 atagombea muhula wa tatu madarakani, uwezekano ambao ulikuwa tayari umechochea maandamano makubwa. Habari hizo zimekuja baada ya Conde kufanikisha mageuzi ya katiba mwezi Machi ambayo wahakiki walihoji kuwa yaliundwa kumuwezesha kugombea tena katika uchaguzi wa Oktoba 18. Taarifa ya chama cha Rally of Guinean People – RPG imesema Conde atakuwa mgombea katika uchaguzi huo. Chama hicho kilimteuwa rasmi mwezi Agosti kugombea, lakini Conde hakuwa ametoa jibu rasmi. Badala yake, aliwaambia wajumbe kuwa RPG lazima kiahidi kuwasaidia wanawake, vijana na watu maskini kabla ya yeye kukubali kugombea katika uchaguzi. Conde alichaguliwa rais katika mwaka wa 2010 na tena katika mwaka wa 2015

Related posts