Macron yuko Lebanon, atoa wito wa kuundwa haraka serikali mpya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito wa kuundwa haraka serikali mpya ya Lebanon kufuatia kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya. Akizungumza baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Beirut, Macron alisema orodha ya maafisa wa serikali mpya inapaswa kutengenezwa haraka iwezekanavyo ili kuinusuru nchi hiyo, ambayo inaendelea kukumbwa na athari za mlipuko mbaya zaidi wa Agosti 4 na kuporomoka kwa uchumi. Ni ziara ya pili ya Macron nchini humo ya kushinikiza haja ya kuufanyia mabadiliko mfumo tata wa kisiasa nchini Lebanon wa misingi ya kidini, tangu mlipuko huo mkubwa uliowauwa watu 188, na kuwajeruhi maelfu ya wengine katika bandari ya Beirut. Aliwasili nchini humo saa chache tu baada ya viongozi kumteuwa Mustapha Adib, mwanadiplomasia mwenye umri wa miaka 48, kuukabili mgogoro mkubwa wa nchi hiyo wa kisiasa na kiuchumi

Related posts