Manyoni (Singida) Mkinichagua Vijiji 2600 nitakamilisha kuviwekea umeme

Mgombea Urais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi 9 (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha anakamilisha Vijiji 2600 vinapatiwa umeme ili kumlika maisha ya watanzania.

Hayo ameyazungumza Wilayani Manyonyi wakati akielekea katika mkutano wa kuomba kura mkoani Singida ili kuteuliwa  kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

“Lengo letu ni kuhakikisha nchi yetu inakuwa ya kisasa ambavyo tunataka watanzania kutoka katika umasikini kwenda katika maisha mazuri ya kila siku” JPM

“Hivyo tusirudi nyuma wanamanyoni na watanzania wote kwa jumla, nipeni awamu nyingine nikafanye maajabu katika kuleta maendeleo ya taifa hili” JPM

Related posts