YOUNG SPIT KUUPELEKA MUZIKI WA BURUNDI DUNIANI

Young Spit Ni Msanii Mwenye Asili Ya Nchini Burundi Ambaye Anafanya Muziki Wa Hiphop Na Ni Moja Kati Ya Msanii Kinda Ambaye Amevutiwa Na Wasanii Wengi Waliofanikiwa Katika Safu Ya Muziki Wa Miondoko Ya Kufoka Yaani Hip Hop Duniani Kote.

Licha Ya Young Spit Kuwa Na Asili Ya Nchini Burundi Lakini Msanii Huyo Ameamua Kuchukua Uraia Wa Marekani Huku Akiwa Anaipeperusha Bendera Ya Kule Alipozaliwa Nazungumzia Nchini Burundi.

Album Yake Ya Kwanza Ilitoka Mnamo Mwaka 2012 Na Album Hiyo Ilikuwa Na Nyimbo  Kama Vile  A Million Dollar Guy,Stunt Hard Na Nyingine Nyingi. Tangu Mwaka 2012 Young Spit Aliendelea Kutoa Nyimbo Tofauti Tofauti Mpaka 2020 Ambapo Msanii Huyo Aliamua Kuachia Album Yake Ya Pili Ambayo Aliipa

Jina La Era 257 Akiwa Ameshirikiana Na Mt Number One,Eddy Jay,Tobi Ali ,Ab Nabil,Gn Nephew Vilevile Album Hiyo In A Nyimbo 10 Ndani Yake  Na Mpaka Sasa Inapatikana Katika Mitandao Mbalimbali Ya Kusambaza Na Kupakua Miziki Kama Vile Spotify ,Deezer,Na Amazon Ambapo Mtu Yeyote Anaweza Kupakua Na Kununua Album Hiyo Iitwayo Era 257.

Mpaka Sasa Young Spit Anaendelea Kuachia Video Za Nyimbo Zake Zinazopatikana Katika Album Hiyo Na Muda Wowote Kuanzia Sasa Ataachia Video Mpya  Ili Kuwa Karibu Na Young Spit Unaweza Kumfuata Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram @Youngspit100 Na Vilevile Unaweza Kuendelea Kusubcribe Katika Chaneli Yake Ya You Tube  Kwa Jina La Young Spit.

Related posts