Aliyewasaidia Wanyarwanda wakati wa Mauaji ya Kimbari akamatwa

Leo September 1, 2020 Taarifa kutokea nchini Rwanda zinasema Paul Rudesabaginaambaye aliwasaidia Wanyarwanda wengi wakati wa Mauaji ya Kimbari kwa kuwahifadhi kwenye Hoteli aliyokuwa anaiongoza amekamatwa. Ujasiri wake ulisababisha kutengenezwa kwa filamu inayoelezea kisa hicho inayofahamika kwa jina la ‘Hotel Rwanda’ Paul anatuhumiwa kwa mashtaka mbalimbali yanayohusiana na makosa ya ugaidi, Mamlaka za Uchunguzi Nchini Rwanda zimeeleza kuwa wamefanikiwa kumkamata Rusesabagina kwa kushirikiana na mataifa mengine bila kuyaweka wazi. Kwa nyakati tofauti, Paul Rusesabagina amekuwa akiikosoa Serikali ya Rais Kagame kwa jinsi ilivyomaliza mgogoro uliopelekea mauaji ya mwaka 1994.

Read More

Kansela Merkel alaani waliovamia jengo la bunge

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amelaani kitendo cha waandamanaji wanaopinga hatua za kudhibiti kusambaa kwa maradhi ya COVID-19, kulivamia jengo la bunge na kukiita kitendo hicho cha ”aibu” akisema wametumia vibaya haki yao ya kuandamana kwa amani. Mamia ya watu walijaribu kulivamia jengo la bunge wakati wa maandamano hayo Mjini Berlin siku ya Jumamosi. Akizungumza na waandishi habari, Msemaji wa Merkel, Steffen Seibert amesema haki muhimu ya kuandamana kwa amani, imekiukwa na waandamanaji. Polisi inakadiria kuwa watu 38,000 walikusanyika mjini Berlin kupinga hatua zilizowekwa kukabiliana na virusi vya corona kama…

Read More