#InstaChocho: “Mama Wawili, Mume Wa Tatu”-Esma Platnumz

HAKIKA hakuna ambaye hakutoa Neno “Hongera” kwa Esma Platnumz ambaye ni Dada Yake na Msanii Wa Bongo Fleva Nchini Tanzania, Diamond Platnumz, baada ya Kubaini kuwa hati maye amefunga Ndoa Tayari na anafurahia maisha hayo Mastaa Wengi sana Nchini tanzania katika Tasnia tofauti za Burudani, hawakusita kumpongeza katika Ukurasa wake wa Instagram baada ya Bibi Esma mwenyewe kudhihirisha kuwa tayari “Pilau” na “Vifijo” tayari vimeshahusika. Ingawa Wengi tulikuwa tukiyafahamu mahusiano yake na mzazi mwenzake “Petiti Man-Wakuache”, Mwanaume aliyefunga Naye ndoa ni mwingine kabisa ambaye wengi hawakudhani na wala hawakuwa wakimfahamu…

Read More

Rapper Jim Jones Achukizwa na Gharama Hii ya Toilet Papers alipoenda Super Market

NCHINI Marekani na baadhi ya Mataifa Mengine huko Ughaibuni, kumekuwa na malalamiko ya kupanda kwa Bei ya “Toilet Papers” katika Super Markets mbali mbali tangu kuwepo kwa maambukizi ya Virusi vya COVID 19 ambavyo husababisha Ugonjwa wa Corona. Katika Mataifa hayo, Baadhi ya Wananchi wamekuwa wakilalamikia sana Bei ya Toilet papers ambayo ilifikia USD 10 sawa na Tsh 23,160/- huku baadhi wakishindwa kabisa kufanya manunuzi ya Bidhaa hizo kwa ajili ya matumizi ya familia na hiyo ni kutokana na kipato chao. Rapper Mkongwe katika Soko la Muziki wa Hip Hop,…

Read More

BOBI WINE: “Ninachojivunia Kuhusu COVID-19, Imefungua Akili za Waganda Wengi Hasa Vijana”

UKIACHILIA mbali suala la Maambukizi ya Virusi ya COVID 19 kuathiri sehemu kadhaa ya Uchumi katika Mataifa mbali mbali ulimwenguni, kuna baadhi ya watu wanaamini kuwepo kwa Virusi hivyo ambavyo husababisha Ugonjwa wa Corona, kumeamsha akili za watu wengi na hata kuibua Maisha halisia ambayo hayakuwa yamezoeleka Mbunge wa Jimbo la Kyadondo Mashariki Nchini Uganda , Joseph Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama “Bobi Wine“, ni mmoja kati ya Watu maarufu ambao wamekuwa wakiichukulia Covid 19 kama sehemu ya kukumbushana mambo ya msingi ambayo hatukuwa tukiyazingatia kabla ya kuwepo kwa Maambukizi ya…

Read More

JIDE JAY DEE: “Nawasihi Msiwe mnaniletea Kolabo Za Mapenzi… Joh Makini Alitetemeka !!”

SIO Mara ya kwanza kusikia kwamba kilichopo nyuma ya kazi nzuri sana ambazo tumekuwa tukizifuatilia, kuzipenda na hata kuzipongeza hasa kutoka kwa Wasanii mbali mbali ulimwenguni, huwa kuna matukio mengi sana ambayo hatuyafahamu na hata tukiyafahamu , basi huwa tunashangaa sana na pengine kubaki tukicheka ama kubaki vinywa Wazi. Ndani ya Wiki Hii, Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya hapa Nchini Tanzania, Judith Wambura maarufu kama “Lady Jay Dee” alikuwa akiadhimisha Siku yake ya Kuzaliwa na alionekana kuwa ni mtu mwenye furaha kubwa sana baada ya kupiga hatua katika umri…

Read More

PROFESA JAY: “Tulianza na Mungu, Tumemaliza na Mungu”

JUMANNE ya Juni 16,2020, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli alivunja Bunge la Tanzania ili kuruhusu Wabunge kurejea katika Majimbo yao tayari kwa taratibu za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba 2020. Katika hatua hiyo, wabunge mbali mbali kupitia vyama vyao na wao wenyewe binafsi walipata kwa nyakati na njia tofauti, walipata nafasi ya kuzungumza mengi kwa wapiga kura wao hasa kupitia vyombo vya habari na hata mitandao ya kijamii hasa kuwashukuru kwa kuwaamini mpaka kufikia hapo walipo hivi…

Read More

YOUNG DEE aanika Ukweli wake Kuhusu MR. BLUE

UKIACHILIA mbali ubora wake katika Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania “Bongo Flava”, Young Dee ni mmoja kati ya Rappers walioanza kupata umaarufu katika Umri mdogo na hata yeye anakiri hilo jambo. Mpaka hivi sasa, Young Dee “Paka Rapper” amezidi kusimama katika ubora wake ambao kila mtu ambaye anafuatilia muziki wa Bongo Fleva anafurahia kila kazi ambayo anaachia kwa mpangilio wake. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Hitmaker huyo wa mkwaju wa “Noma Kweli” ameweka bayana safari yake ya muziki ilipoanzia na kufikia hapo alipo, huku akiwataja na kuwashukuru watu ambao…

Read More

KINGWENDU: “Mwanza Vijijini Kumesababisha Tusifanye Filamu za Vichekesho”

KAMA utakuwa unakumbuka vizuri sana, kipindi cha Nyuma Filamu nyingi sana za Vichekesho zilikuwa ni sehemu ya Gumzo na hata kufikia hatu kupendwa sana na wadau wengi sana wa tasnia hiyo hapa Nchini Tanzania. Katika filamu hizo, ulikuwa unakutana na muunganiko wa wasanii wengi sana wa vichekesho, hali ambayo iliashiria kuwa huenda umoja wao ukaendelea kutpatia burudani na wao kupata matunda kutokana na kuwepo kwa mauzo mengi mitaani. KINGWENDU ni miongoni mwa wachekeshaji wakongwe ambao pia walionekana sana katika Filamu hizo za vichekesho na kuleta ladha nzuri sana huku akishirikiana…

Read More

QUEEN LATIFAH: “Vijana, Huu Sio Mwisho Wa Dunia. Hii Ni Dunia Yenu”

UKIACHILIA mbali uwezo wake mkubwa wa uandishi wa mashairi “Konki” katika muziki wa Hip Hop, Ufundi wake “Mtamu” kwenye suala zima la “Ku-flow” kunako Kazi zake na hata zile ambazo anashirikishwa, Mkongwe kwenye utamaduni wa “hip Hop” Duniani kwa upande wa Jinsia ya Kike, Queen Latifah pia ni miongoni mwa Waigizaji Bora sana katika ulimwengu wa filamu Duniani na kila mtu analiheshimu hilo kwa nafasi yake. Lakini nje ya Vipaji hivyo alivyonavyo, Queen Latifah pia ni miongoni mwa Wasanii ambao waliamua kusimama katika upande wa Harakati za kimaendeleo hasa kwa…

Read More

LUDACRIS: “Niliongea na Familia Ya George Floyd”

RAPA Ludacris ni Miongoni mwa watu maarufu ambao waliungana na Familia ya Marehemu George Floyd Nchini Marekani, katika Msiba sambamba na Mazishi, ikiwa ni sehemu ya kuguswa na kitendo cha “kikatili” kilichofanywa na Baadhi ya Askari Polisi ambao walipelekea Kifo cha Mmarekani mweusi huyo. Ukiachilia mbali kuhusika ama kujumuika na Familia ya marehemu, Ludacris pia aliungana na maelfu ya raia wa Marekani ambao walikuwa katika maandamano ya kupiga vita Ubaguzi wa rangi ambao umekuwa ukisababisha vifo vya “wamarekani Weusi” na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo George Floyd ambaye alipoteza…

Read More

#Mnazingua: MEGHAN THEE STALLION Hajapenda hili kutoka kwa Wamiliki wa Instagram !!

KIUHALISIA Sio kila mtu huwa anapenda Mabadiliko ama maboresho ya aina tofauti katika “App” mbali mbali hasa za mitandao ya Kijamii. Lakini pia, sio kila mtu huwa anachukia maboresho ya “app” hizo za mitandao ya kijamii. Meghan Thee Stallion, ni mmoja kati Ya watu wachache ambao pengine hawajafurahishwa na mabadiliko mapya katika “account” yake ya Instagram na kuamua kuwapa “makavu” wamiliki na hata mafundi wanaoshughulikia mabadiliko katika mtandao huo. Rapa huyo wa kike ambaye hivi sasa anafanya Vema na mkwaju wa “Savage Remix” aliomshirikisha bibie Beyonce, amechukizwa haswa na mamboresho…

Read More