VIDEO: Rais Dkt. John Pombe Magufuli akutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dkt. Hafez Ghanem ambaye ametangaza kuwa Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya Sekondari

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dkt. Hafez Ghanem ambaye ametangaza kuwa Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya Sekondari Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

Basi la kampuni BM COACH linalofanya safari zake kati ya Morogoro – Kilimanjaro limepata ajali

Basi la kampuni BM COACH linalofanya safari zake kati ya Morogoro – Kilimanjaro limepata ajali wakati linashuka mteremko wa Mto Wami mita chache kabla ya daraja. – Kwa mujibu wa taarifa za awali hakuna majeruhi wala vifo katika ajali hiyo isipokuwa abiria wamepata mshtuko na taharuki – Ajali hiyo imesababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa breki hali iliyopelekea basi hilo ligonge Lori lililokuwa kando ya barabara – Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

MAJAMBAZI SABA WAUWAWA NA POLISI MWANZA

Watu saba wanaosadikika kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na jeshi la polisi jijini Mwanza. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kishiri. Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

WALAZIMIKA KUTEMBEA KWA MGUU KWENDA KAZINI, NI BAADA YA MAGARI YA ABIRIA KUGOMA

Mamilioni ya wasafiri kote nchini Kenya leo wamelazimika kutembea kwa mwendo mrefu hadi sehemu zao za kazi ama kutumia njia mbadala za usafiri baada ya magari ya uchukuzi wa umma ya matatu au daladala kususia kuhudumu. Wamiliki wa matatu wanapinga hatua ya serikali kutekeleza sheria kali za kudhibiti usalama wa abiria. Sheria hii inawataka wamiliki wa matatu waweke mikanda ya usalama, vidhibiti mwendo vya kidijitali na magari yote yawe na dereva na wahudumu walioajiriwa. Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

U.S.A: Chama cha rais Donald Trump, Republicans kimepoteza wingi katika bunge la Congress:

Chama cha rais Donald Trump, Republicans kimepoteza wingi katika bunge la Congress hali ambayo itafanya muda uliosalia wa urais wa Trump kupitia wakati mgumu zaidi. Republicans pia wamepoteza viti saba vya Ugavana mpaka sasa. Hata hivyo chama hicho kimefanikiwa kubaki na wingi katika bunge la Seneti. Kwenye uchaguzi wa bunge la Congress, mpaka sasa majimbo 412 yametangaza matokeo. Democrats wanaongoza kwa viti 219 huku Republicans wakifuatia na viti 193. #chanzobbcswahili Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

SITA WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI PWANI

  Watu sita wamefariki dunia katika Kijiji cha Msata baaada ya gari aina ya Toyota Coster lenye namba za usajili T.124DHW iliyokuwa ikitokea Mkata kwenda Mbezi Dar es Salaam kugongana na Lori lenye namba za usajili KBV 746C/ZE2861 FAW. Kamanda wa police Mkoa wa Pwani Wankyo Nyegesa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo . Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

MAMA AMUUA MWANAE KWA KIPIGO AKIMTUHUMU KUIBA MAEMBE KWA JIRANI,

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye RAHEL MATALAKA, miaka 41, mkazi wa kijiji cha lugenge, kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto wake wa kiume aitwaye MALIATABU CONSTANTINE, miaka 10, mwanafunza wa darasa la pili shule ya msingi Ikeleg,Wilayani Misungwi. Tukio hilo la mauaji limetokea tarehe 03.11.2018 majira ya 1:00 jion, hii ni baada ya mama wa marehemu kupokea malalamiko kuwa mtoto wake alikua akiangusha na kuiba maembe kwa jirani. Ndipo mtuhumiwa alipatwa na hasira na kumpiga mtoto kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili…

Facebook Comments

Read More

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKOJOLEA DUKA LA MKEWE, MWENYEWE ADAI LENGO NI KUMLAANI MKEWE ALIYEMNYIMA CHAKULA

  Mwanume mmoja Simon Wachira (53) mkazi wa eneo la Mikindani kaunit ya Mombasa nchini Kenya ambaye anatajwa kuwa mlevi wa kupindukia amefikishwa mahakamani kwa kosa la kukojoa mbele ya duka la mkewe. Mwanume huyo anadaiwa kutenda kisa hicho 23 October mwaka huu kwa lengo la kumlaani mkewe na watoto wake waliokataa kumpa chakula ili hali anjaa kabla ya kufikishwa mahakamani Jumanne 30 October mwaka huu . Akijitetea mbele ya hakimu mkuu Julius Nange’a, Wachira alikiri kutekeleza kitendo hicho cha aibu na kusema kuwa nia yake ilikuwa ni kumlaani mkewe…

Facebook Comments

Read More

MSICHANA ATISHIA KUJIUA ENDAPO ATALAZIMISHWA KUENDELEA NA MASOMO

Mwanafunzi mmoja wa kike (15) wa kidato cha kwanza amenusurika kufa kwa kujinyonga baada ya kukerwa na wazazi wake wanaomlazimisha aendelee na masomo. Msichana huyo wa shule ya Sekondari Nsemlwa, Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi amefikia uamuzi huo ili asisumbuliwe na wazazi wake wakati yeye hataki kusoma. Siku ya tukio msichana huyo anadaiwa kuandaa kitanzi na stuli ili atekeleze mpango huo kabla ya kuokolewa na baba yake mzazi Bushiri Joseph ambaye alimkuta tayari amepanda kwenye kiti hicho. Mwanafunzi huyo pamoja  mwenzake wa kiume mwenye umri wa miaka 16, anayesoma kidato cha pili…

Facebook Comments

Read More

ALIYEMUWEKA MWANAFUNZI KINYUMBA MATATANI

  Bwana mmoja mkazi wa Nansimo wilaya ya Bunda mkoani Mara huenda akakabiliwa na kifungo cha miaka thelathini jela baada ya kubainika kumuweka mwanafunzi kinyumba. Bwana huyo anadaiwa kutenda kisa hicho kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Mwibara iliyopo wilayani humo. Mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia Bupilipili aliagiza kukamatwa kwa mwanaume huyo baada ya kufika shuleni hapo na kubaini kisa hicho. Bupilipili alisema kila mwananchi anapaswa kuungana na serikali kutokomeza vitendo hivyo. Facebook Comments

Facebook Comments

Read More