KUNGUNI WAFUNGA MAHAKAMA !

MAHAKAMA ya jimbo la ROGERS, Oklahoma Nchini Marekani, imelazimika kusitisha Shughuli za Kimahakama baada ya kubainika kwa Kunguni ndani ya Mahakama Hiyo Kunguni hao walionekana wakidondoka kutoka katika Moja ya Vazi la Mwanasheria aliyekuwa katika Mahakama hiyo wakati shughuli za kimahakama zikiendelea, hli iliyosababisha Uongozi kuchukua Jukumu la kufunga mahakama mpaka hali itakapokuwa Sawa. Akifafanua kuhusu hali hiyo, Mmoja wa Viongozi katika utawala wa Jimbo hilo ambaye pia alipewa jukumu la kutoa ufafanuzi juu ya hatua hiyo, SCOTT WALTON ameweka bayana kuwa mwanasheria huyo alifika katika Ghorofa ya Tatu ambako…

Facebook Comments

Read More

AMSHITAKI BABA YAKE KWA KUTOMJENGEA CHOO

Msichana wa miaka saba nchini India amemshitaki baba yake polisi baada ya kushindwa kutekeleza ahadi aliyomuahidi. Hanifa Zaara amewaambia polisi kuwa baba yake amekua akimdanganya na kuwataka akamatwe na kushtakiwa. Msichana huyo amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya baba yake kushindwa kutimiza ahadi ya kumjengea choo na kwamba amekuwa akiona aibu kwenda haja vichakani kwa kukosa choo. Hanifa ambaye anaishi na wazazi wake katika mji wa Ambur, jimboni Tamil Nadu, anasema hajawahi kuona choo nyumbani kwao huku katika mtaa anaoishi ni majirani wachache tu ndio wana vyoo majumbani mwao…

Facebook Comments

Read More

MCHUNGAJI ASHAMBULIWA KWA MAWE AKITUHUMIWA KWA UCHAWI MKOANI KATAVI

Wananchi wakiwemo Waumini wavamia nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Sauti ya Uzima, Elia Zabron Balashika(36) maarufu ‘Nabii Elia’ raia wa Burundi na kuishambulia kwa mawe – Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Damas Nyanda alisema tukio hilo lilitokea Mtaa wa Kazima Ringini Manispaa ya Mpanda ambapo Mchungaji huyo amekuwa akitoa huduma kwa miaka sita katika eneo hilo – Chanzo ni imani za ushirikina baada ya taarifa kuzagaa kuwa Nabia Elia aliweka ‘misukule’ watano nyumbani kwake ambao waumini wa kanisa walimtaka awatoe hadharani – Taarifa zilitolewa Polisi ambapo walifika eneo la…

Facebook Comments

Read More

Mwanaharakati Nchini India, Mbaroni kwa picha ya Utupu

Mahakama moja nchini India 🇮🇳 imeamrisha mwanaharakati wa kihindi bi Rehana Fathima kukaa rumande siku 14 kwa kuchapisha picha hii ☝🏿kwenye mtandao wa Facebook. Polisi wanasema picha hii ni ya ”utupu”. Amewekwa rumande kwa siku 14 kuruhusu polisi wakamilishe uchunguzi. Je picha hii ya utupu? #chanzobbcswahili Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

AMUUA MKEWE KWA PANGA,NI BAADA YA KUMFUMANIA NA MWANAUME MWINGINE CHUMBANI KWAKE

  Mwanaume mmoja Paul Maritim ameripotiwa kumuua mkewe kwa kumchinja shingoni kwa panga baada ya kumkuta akifanya mapenzi na mwanaume mwingine chumbani kwao. Mbali na mauaji hayo pia mwanaume huyo mkazi wa kijiji cha Kapregerego kaunti ya Nakuru nchini Kenya anadaiwa kumjeruhi kwa mapanga mwanaume aliyemfumania na mkewe wakifanya tendo hilo. Siku ya tukio Maritimu alirejea nyumbani kwake na kumfumania mkewe akiwa na mwanaume chumbani kwake jambo lilimghadhabisha na kuamua kuchukua panga na kuwashambulia. Majirani waliofika katika eneo la tukio kushuhudia kilichokuwa kikiendelea, inasemekana walifurushwa na Maritim huku akitishia kuwakatakata…

Facebook Comments

Read More

AUWA MTOTO KWA KUMTUPA CHOONI NA KUTOKOMEA

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka arobaini anasakwa na polisi kwa kosa la kumtupa mtoto wake chooni. Inadaiwa mwanamke huyo aliyeshirikiana na mumewe kabla ya kutenda kisa hicho alimtaarifu daktari kuwa angefanya hivyo muda mchache baada ya kujifungua. Kisa hicho kimeripotiwa kutokea katika eneo la kijiji cha Kibingo eneo la Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya. Mwanamke huyo anadaiwa kutenda kisa hicho na kutokomea. Awali daktari aliwafahamisha watu kuwa makini mno na mwanamke huyo lakini kwa bahati mbaya, aliutekeleza unyama huo Visa vya wanawake kuwatupa watoto wao vimekuwapo kwa muda mrefu…

Facebook Comments

Read More

ABAKWA NA WANAUME WAWILI NJIANI AKIELEKEA KUJIFUNGUA

  Mwanamke mmoja mjamzito ameripotiwa kubakwa na wanaume wawili mbele ya watoto wake akiwa njian kwenda hospitali kujifungua. Mjamzito huyo kutoka mtaa wa Huruma jijini nairobi siku ya tukio akiwa na mwanaye walikutana na wanaume hao waliowachukua kwa nguvu hadi vichakani na kumbaka bila kujali hali yake mbele ya mwanaye. Wabakaji hao walidaiwa kumtishia mama huyo kumuua endapo atatoa taarifa polisi. Tayari maafisa wa polisi wamefanikiwa kumtambua mmoja wa washukiwa hao wa ubakaji aitwaye Kamau au kwa jina la utani Kamare ambaye anaishi na mjombake katika eneo la Mlango Kubwa…

Facebook Comments

Read More

APONZWA NA KITABU CHA NGONO ,SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA KUMI GEREZANI

Mwandishi mmoja wa vitabu nchini Uchina amefungwa miaka 10 jela kwa kuandika na kuuza kitabu chenye maudhui ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja. Mwandishi huyo mwanamke afahamikaye kwa jina la Liu, alihukumiwa kifungo hicho na na mahakama ya jimbo la Anhui mwezi uliopita kwa kuuza “maudhui machafu”. Jina la kitabu hicho ni “Occupation”, lenye maana ya kazi kwa kiswahili na kimebeba maudhui ya “tabia ya ngono ya wapenzi wa jinsia noja wa kiume…pamoja na aina za kupotosha za ngono na kwenda kinyume na jamii.” Kwa mujibu wa shirika la…

Facebook Comments

Read More

WAHUBIRI WATWANGANA MAKONDE WAKIGOMBEA SADAKA KWENYE BASI

  Abiria katika gari moja la usafiri wa uma (daladala) walibaki vinywa wazi baada ya wahubiri wawili kutwangana makonde kila mmoja akitaka awahubirie abiria hao na kukusanya sadaka. Kisa hicho kilitokea katika gari moja la abiria katika eneo la Kiritiri Embu nchini Kenya baada ya muhubiri mmoja kuingia katika gari hilo na kutaka ahubiri hali ya kuwa tayari mwenzake alishaanza kuhubiri abiria hao. ”Sasa mbona unakuja kuhubiri hapa ilhali unaona nishaingia na kuanza kusoma Biblia. Toka nje na uende ukahubiri kwa gari jingine,’’ mmoja alimwambia mwenzake. ‘’ Hakuna yule ambaye…

Facebook Comments

Read More

Basi la kampuni BM COACH linalofanya safari zake kati ya Morogoro – Kilimanjaro limepata ajali

Basi la kampuni BM COACH linalofanya safari zake kati ya Morogoro – Kilimanjaro limepata ajali wakati linashuka mteremko wa Mto Wami mita chache kabla ya daraja. – Kwa mujibu wa taarifa za awali hakuna majeruhi wala vifo katika ajali hiyo isipokuwa abiria wamepata mshtuko na taharuki – Ajali hiyo imesababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa breki hali iliyopelekea basi hilo ligonge Lori lililokuwa kando ya barabara – Facebook Comments

Facebook Comments

Read More