AMUUA MKEWE KWA PANGA,NI BAADA YA KUMFUMANIA NA MWANAUME MWINGINE CHUMBANI KWAKE

  Mwanaume mmoja Paul Maritim ameripotiwa kumuua mkewe kwa kumchinja shingoni kwa panga baada ya kumkuta akifanya mapenzi na mwanaume mwingine chumbani kwao. Mbali na mauaji hayo pia mwanaume huyo mkazi wa kijiji cha Kapregerego kaunti ya Nakuru nchini Kenya anadaiwa kumjeruhi kwa mapanga mwanaume aliyemfumania na mkewe wakifanya tendo hilo. Siku ya tukio Maritimu alirejea nyumbani kwake na kumfumania mkewe akiwa na mwanaume chumbani kwake jambo lilimghadhabisha na kuamua kuchukua panga na kuwashambulia. Majirani waliofika katika eneo la tukio kushuhudia kilichokuwa kikiendelea, inasemekana walifurushwa na Maritim huku akitishia kuwakatakata…

Read More

AUWA MTOTO KWA KUMTUPA CHOONI NA KUTOKOMEA

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka arobaini anasakwa na polisi kwa kosa la kumtupa mtoto wake chooni. Inadaiwa mwanamke huyo aliyeshirikiana na mumewe kabla ya kutenda kisa hicho alimtaarifu daktari kuwa angefanya hivyo muda mchache baada ya kujifungua. Kisa hicho kimeripotiwa kutokea katika eneo la kijiji cha Kibingo eneo la Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya. Mwanamke huyo anadaiwa kutenda kisa hicho na kutokomea. Awali daktari aliwafahamisha watu kuwa makini mno na mwanamke huyo lakini kwa bahati mbaya, aliutekeleza unyama huo Visa vya wanawake kuwatupa watoto wao vimekuwapo kwa muda mrefu…

Read More

ABAKWA NA WANAUME WAWILI NJIANI AKIELEKEA KUJIFUNGUA

  Mwanamke mmoja mjamzito ameripotiwa kubakwa na wanaume wawili mbele ya watoto wake akiwa njian kwenda hospitali kujifungua. Mjamzito huyo kutoka mtaa wa Huruma jijini nairobi siku ya tukio akiwa na mwanaye walikutana na wanaume hao waliowachukua kwa nguvu hadi vichakani na kumbaka bila kujali hali yake mbele ya mwanaye. Wabakaji hao walidaiwa kumtishia mama huyo kumuua endapo atatoa taarifa polisi. Tayari maafisa wa polisi wamefanikiwa kumtambua mmoja wa washukiwa hao wa ubakaji aitwaye Kamau au kwa jina la utani Kamare ambaye anaishi na mjombake katika eneo la Mlango Kubwa…

Read More

APONZWA NA KITABU CHA NGONO ,SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA KUMI GEREZANI

Mwandishi mmoja wa vitabu nchini Uchina amefungwa miaka 10 jela kwa kuandika na kuuza kitabu chenye maudhui ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja. Mwandishi huyo mwanamke afahamikaye kwa jina la Liu, alihukumiwa kifungo hicho na na mahakama ya jimbo la Anhui mwezi uliopita kwa kuuza “maudhui machafu”. Jina la kitabu hicho ni “Occupation”, lenye maana ya kazi kwa kiswahili na kimebeba maudhui ya “tabia ya ngono ya wapenzi wa jinsia noja wa kiume…pamoja na aina za kupotosha za ngono na kwenda kinyume na jamii.” Kwa mujibu wa shirika la…

Read More

WAHUBIRI WATWANGANA MAKONDE WAKIGOMBEA SADAKA KWENYE BASI

  Abiria katika gari moja la usafiri wa uma (daladala) walibaki vinywa wazi baada ya wahubiri wawili kutwangana makonde kila mmoja akitaka awahubirie abiria hao na kukusanya sadaka. Kisa hicho kilitokea katika gari moja la abiria katika eneo la Kiritiri Embu nchini Kenya baada ya muhubiri mmoja kuingia katika gari hilo na kutaka ahubiri hali ya kuwa tayari mwenzake alishaanza kuhubiri abiria hao. ”Sasa mbona unakuja kuhubiri hapa ilhali unaona nishaingia na kuanza kusoma Biblia. Toka nje na uende ukahubiri kwa gari jingine,’’ mmoja alimwambia mwenzake. ‘’ Hakuna yule ambaye…

Read More

Basi la kampuni BM COACH linalofanya safari zake kati ya Morogoro – Kilimanjaro limepata ajali

Basi la kampuni BM COACH linalofanya safari zake kati ya Morogoro – Kilimanjaro limepata ajali wakati linashuka mteremko wa Mto Wami mita chache kabla ya daraja. – Kwa mujibu wa taarifa za awali hakuna majeruhi wala vifo katika ajali hiyo isipokuwa abiria wamepata mshtuko na taharuki – Ajali hiyo imesababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa breki hali iliyopelekea basi hilo ligonge Lori lililokuwa kando ya barabara –

Read More

MSICHANA ATISHIA KUJIUA ENDAPO ATALAZIMISHWA KUENDELEA NA MASOMO

Mwanafunzi mmoja wa kike (15) wa kidato cha kwanza amenusurika kufa kwa kujinyonga baada ya kukerwa na wazazi wake wanaomlazimisha aendelee na masomo. Msichana huyo wa shule ya Sekondari Nsemlwa, Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi amefikia uamuzi huo ili asisumbuliwe na wazazi wake wakati yeye hataki kusoma. Siku ya tukio msichana huyo anadaiwa kuandaa kitanzi na stuli ili atekeleze mpango huo kabla ya kuokolewa na baba yake mzazi Bushiri Joseph ambaye alimkuta tayari amepanda kwenye kiti hicho. Mwanafunzi huyo pamoja  mwenzake wa kiume mwenye umri wa miaka 16, anayesoma kidato cha pili…

Read More