PROFESA JAY: “Tulianza na Mungu, Tumemaliza na Mungu”

JUMANNE ya Juni 16,2020, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli alivunja Bunge la Tanzania ili kuruhusu Wabunge kurejea katika Majimbo yao tayari kwa taratibu za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba 2020. Katika hatua hiyo, wabunge mbali mbali kupitia vyama vyao na wao wenyewe binafsi walipata kwa nyakati na njia tofauti, walipata nafasi ya kuzungumza mengi kwa wapiga kura wao hasa kupitia vyombo vya habari na hata mitandao ya kijamii hasa kuwashukuru kwa kuwaamini mpaka kufikia hapo walipo hivi…

Read More

MAANDAMANO yaibuka Nchini TUNISIA

Muungano mkubwa zaidi wa wafanyakazi nchini Tunisia UGTT umesema mgomo wa nchi nzima wa watumishi wa umma Zaidi ya LAKI MOJA umeanza hii leo Alhamisi. Mgomo huo ni wa kushinikiza serikali ya Tunisia iwape nyongeza ya mishahara wafanyakazi wa umma wapatao laki sita na 70 elfu. Mgomo huo umeathiri zaidi huduma katika viwanja vya ndege, mashule na hata shirika la habari la serikali. Mgomo huo wa wafanyakazi wa serikali umeanza katika hali ambayo, Tunisia kwa siku kadhaa sasa imekuwa ikishuhudia maandamano ya wananchi wakilalamikia utendaji wa serikali na hali mbaya…

Read More

MARUFUKU kuvaa Mavazi Yenye Rangi NYEKUNDU Uganda

WATU watakaobainika kuwa wamevaa Nguo Nyekundu, Kofia Nyekundu na Kitambaa chekundu Katika wilaya ya LAMWO nchini Uganda, watakiona “cha Mtema Kuni” kutoka kwa jeshi la Polisi maana watakuwa wanaashiria kuunga mkono chama cha People’s Power. Agizo hilo limetoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, (RDC) James Nabinson Kidega ambaye amelipatia mamlaka Jeshi la polisi Katika wilaya hiyo kuhakikisha kuwa linakamata Mavazi hayo ambayo yanauzwa ama kupatia watu ambao wanamuunga Mkono Msanii wa Uganda ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kama “Bobi Wine” Tofauti na hilo, Bw. Kidega…

Read More

Kuelekea uchumi wakati na Tanzania ya viwanda Watanzania kunufaika na viwanda 3300

Kuelekea uchumi wakati na Tanzania ya viwanda watanzania wameelezwa kunufaika na viwanda 3300 vilivyosajiliwa hapa nchini. Hayo yamebainishwa na msemaji wa serikali Hassan Abass wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupitia Radio jembe katika kipindi maalum akifafanua utendaji kazi wa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa miaka mitatu madarakani Amesema mpaka sasa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wameshajisajili katika uanzishwaji wa mradi huo wa viwanda ikiwa kuna viwanda vikubwa ,vya kati na vidogo ambavyo vitaweza kuwanufaisha watanzania katika nyanja mbalimbali hasa ajira Aidha dr Abass ameeleza…

Read More

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekiri kuwa alidanganya wabunge

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekiri kuwa alidanganya wabunge waliokuwa wanachunguza ufisadi serikalini aliposema kuwa dola $35,000 zilizotumwa kwa akaunti yake kutoka kampuni ya Bosasa, zilikuwa ni malipo kwa ushauri wa mwanaye Andile. Hata hivyo uchunguzi umebaini pesa hizo zilikuwa mchango kwa kampeni yake. Malipo hayo yakifanyika punde baada ya Kampuni hiyo kushinda zabuni kubwa ya serikali. Je kampeini ya rais Ramaphosa dhidi ya rushwa na ufisadi imeingia doa?

Read More

U.S.A: Chama cha rais Donald Trump, Republicans kimepoteza wingi katika bunge la Congress:

Chama cha rais Donald Trump, Republicans kimepoteza wingi katika bunge la Congress hali ambayo itafanya muda uliosalia wa urais wa Trump kupitia wakati mgumu zaidi. Republicans pia wamepoteza viti saba vya Ugavana mpaka sasa. Hata hivyo chama hicho kimefanikiwa kubaki na wingi katika bunge la Seneti. Kwenye uchaguzi wa bunge la Congress, mpaka sasa majimbo 412 yametangaza matokeo. Democrats wanaongoza kwa viti 219 huku Republicans wakifuatia na viti 193. #chanzobbcswahili

Read More

ZITO AACHIWA KWA DHAMANA, NI BAADA YA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

  Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe (ACT) ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka matatu ikiwemo kutoa maneno ya uchochezi na kuyakana yote. Kwa mujibu wa Wakili wake, Jebra Kambole, Zitto ameyakana mashtaka yote matatu na kesi imeahirishwa hadi Novemba 26 mwaka huu. Masharti ya dhamana ilikuwa ni kuwa na mdhamini mmoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 10.

Read More

KAMATI KUU CHADEMA YAWACHUKULIA HATUA KUBENEA NA MWENZAKE

Kamati Kuu ya Chadema, imewavua nafasi zote za Uongozi na kuwaweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, Saed Kubenea na Anthony Komu baada ya kukiri kusambaza sauti iliyolenga kudhohofisha chama. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika amesema, katika uamuzi huo wa Kamati Kuu, wabunge hao wamekiri makosa yao katika mkutano walioitwa mbele ya kamati na kuomba radhi kama walivyotakiwa kufanya. Kwa mujibu wa Mnyika, wabunge hao pia wamevuliwa nyazifa zao ndani ya chama na kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi 12.

Read More