LUDACRIS: “Niliongea na Familia Ya George Floyd”

RAPA Ludacris ni Miongoni mwa watu maarufu ambao waliungana na Familia ya Marehemu George Floyd Nchini Marekani, katika Msiba sambamba na Mazishi, ikiwa ni sehemu ya kuguswa na kitendo cha “kikatili” kilichofanywa na Baadhi ya Askari Polisi ambao walipelekea Kifo cha Mmarekani mweusi huyo. Ukiachilia mbali kuhusika ama kujumuika na Familia ya marehemu, Ludacris pia aliungana na maelfu ya raia wa Marekani ambao walikuwa katika maandamano ya kupiga vita Ubaguzi wa rangi ambao umekuwa ukisababisha vifo vya “wamarekani Weusi” na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo George Floyd ambaye alipoteza…

Read More

UJUMBE WA AUNTY EZEKIEL KWA BINTI YAKE: “Naomba Kwa Hapa tulipofikia Mwanangu, Utanisamehe……. “

BINTI wa Kike wa Muigizaji wa Filamu hapa nchini Tanzania (Bongo Movie), Aunty Ezekiel, ambaye anaitwa “Cookie” hatimaye amepiga hatua nyingine katika maisha yake hasa kwa kuongeza Umri mwingine, akiwa mwenye afya nzuri na tabasamu Mwanana. Hiyo imethibitishwa kupitia instagram account ya Mama yake (aunty Ezekiel) ambaye aliandka ujumbe mrefu ulikuwa na maelezo ambayo kila mtu amebaki na uelewa wake katika tafsir yake kulingana na namna ambvyo Aunty mwenyewe aliandika ujumbe huo na kusomwa na maelfu ya Wafuasi wake Katika Ujumbe huo, Aunty ameelezea namna ambavyo amejitoa vilivyo kuhakikisha Cookie…

Read More

#ChukiNjeNje: Rapa 50 Cents Afafanua kuhusu “Bifu” lililopo Baina Yake na Mtoto wake Mkubwa !!

RAPA Jackson “50 Cents” Curtis ambaye pia ni Hit Maker wa Track ya “In Da Club”, amethibitisha namna ambavyo hampendi tena Mtoto wake Mkubwa, Marquise Jackson kama ilivyokuwa mwanzo. Akizungumza kupitia Instagram Live, 50 Cents amekiri kutokuwepo na maelewano mazuri na mtoto wake huyo kwa muda mrefu sasa, huku akitoa lawama kubwa kwa mzazi mwenzake ambaye ni mama mzazi wa Kijana wao kuwa yeye ndiye chanzo cha “sumu” kubwa iliyoko baina yao wawili. 50 Cents ambaye hivi majuzi ameachia kitabu chake chenye jina la “Hustle Harder, Hustle Smarter” amekiri kabisa…

Read More

JUA CALI: “Haukwepo Ugomvi kati ya OGOPA DJs na CALIF RECORDS”

MIAKA Ya Nyuma Nchini Kenya katika Muziki wa Kizazi kipya, kumewahi kutokea Ushindani mkubwa baina ya Records Labels mbili ambazo ni CALIF RECORDS na OGOPA Djs, hali ambayo ilikuja kutafsirwa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa na kutokuelewana baina ya Pande hizo mbili. JUA CALI ambaye ni msanii mkongwe aliyefanikiwa kuufanya Muziki wa “Genge” ufike mahali pakubwa Nchini humo, amefafanua kuhusu Tetesi hizo ambazo mpaka leo kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa Label hizo zimewahi kuwa na Ugomvi mkubwa sana JUA CALI ambaye alikuwa chini ya Records Label ya CALIF amesema…

Read More

RC MGHWIRA : “Ninajua Kuimba, Nyimbo za Corona Zipo”

MARA Nyingi viongozi wengi wa Kiserikali, wamekuwa sio wepesi kuonesha upande wao wa pli katika Maisha yao hasa linapokuja suala “Vipaji”. Pengine hii hutokana na majukumu mengi katika Sekta zao, lakini hata namna ambavyo wamekuwa wakitengeneza taswira zao za kimajukumu hasa kwa wananchi wao. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira ni mmoja kati ya Viongozi wa Kiserikali ambaye hakusita kuonesha uwezo wake wa Kuimba ikiwa ni moja kati ya kutumia njia hiyo ili kufikisha ujumbe kuhusu kuwepo kwa maambukizi ya Virusi vya Corona. Mheshimiwa Mghwira ameongeza kuwa, yeye…

Read More

VICTORIA KIMANI : “Huu Ni Muda wa Kuipa Nafasi Digitali”

Katika Ulimwengu wa Burudani, Wasanii mbali mbali na wadau husika wamekuwa katika wakati mgumu hasa kiuchumi kutokana na Kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona. Hii inatokana na ushauri wa Wataalamu wa Afya na Viongozi mbali mbali Duniani kusihi watu kuepukana na Mikusanyiko ya Watu ili kuzuzia kusambaa kwa Virusi hivyo. Nchini Kenya, hivi sasa hakuna matamasha ya Burudani kama ilivyokuwa awali, na hii inatokana na agizo la Serikali ya Nchi hiyo kuwasihi watu kutulia Nyumbani na kuepusha misongamano ya Watu katika maeneo mbali mbali. Victoria Kimani, mmoja kati ya…

Read More

WMO Wathibitisha Kuwa Viwango vya Joto Vinapanda

Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa duniani, WMO limesema ongezeko la viwango vya joto ni ishara ya wazi ya mabadiliko ya tabia-nchi ya muda mrefu, huku wakifafanua kuwa miaka minne iliyopita viwango vilikuwa vya kipekee. WMO katika taarifa imesema miaka¬†katika ya 2015, 2016, 2017 na 2018 kumekuwa na Joto Kubwa na hiyo ni ishara ya wazi kuwa mabadiliko ya tabia-nchi yanaendelea. Akizungumzia mwenendo wa hali ya hewa, Katibu Mkuu wa WMO, Petteri Taalas amesema mwenendo wa muda mrefu ni muhimu kuliko uchunguzi wa mwaka mmoja mmoja na…

Read More

YOGO BEATS : “UKINILIPA VIZURI, NITAFANYA KAZI YAKO” (AUDIO)

SINA hakika kama kuna mtu ambaye atakidhi kiu yako kiufasaha zaidi hasa katika Nyanja ya Kazi, kama utampa malipo ambayo hayaridhishi hata kidogo, na hiyo ipo kwa Watu Wengi Sana Wengi tulianza kumuelewa Zaidi Producer YOGO BEATS baada ya kuanza kufanya Kazi na NEDY MUSIC kupitia Tracks kadha wa kadha hasa ikiwemo NISHALEWA na ONE AND ONLY. Tofauti na hilo, Ndiye Producer ambaye amemfanya Msaii huyo kujipatia Tuzo ya kimataifa ambayo imemuweka katika Ramani Nzuri sana ya Muziki wa kimataifa Tofauti na Producers wengine, YOGO BEATS hana njaa ya kutengeneza…

Read More

KUNGUNI WAFUNGA MAHAKAMA !

MAHAKAMA ya jimbo la ROGERS, Oklahoma Nchini Marekani, imelazimika kusitisha Shughuli za Kimahakama baada ya kubainika kwa Kunguni ndani ya Mahakama Hiyo Kunguni hao walionekana wakidondoka kutoka katika Moja ya Vazi la Mwanasheria aliyekuwa katika Mahakama hiyo wakati shughuli za kimahakama zikiendelea, hli iliyosababisha Uongozi kuchukua Jukumu la kufunga mahakama mpaka hali itakapokuwa Sawa. Akifafanua kuhusu hali hiyo, Mmoja wa Viongozi katika utawala wa Jimbo hilo ambaye pia alipewa jukumu la kutoa ufafanuzi juu ya hatua hiyo, SCOTT WALTON ameweka bayana kuwa mwanasheria huyo alifika katika Ghorofa ya Tatu ambako…

Read More

RAIS WA SUDAN : ” MILANGO IKO WAZI KWA WAANDAMANAJI KUFANYA MAZUNGUMZO”

Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesema mlango wa mazungumzo utaendelea kuwa wazi kwa waandamanaji vijana ambao wanaingia mitaani kuandamana kwa Madai ya hali mbaya ya uchumi na kutumia mgogoro wa Sudan Kusini kama chanzo kikuu cha mgogoro wa kiuchumi nchini Sudan. Al-Bashir amebainisha kuwa, Mgogoro wa Sudani Kusini ni sababu kubwa ya kuzorota kwa uchumi wa Sudan. Sudan imekuwa ikisumbuliwa na migogoro katika historia yake licha ya makubaliano ya amani uliosainiwa mwaka 2015. Serikali za kusini zilisalia na kuunda Jamhuri ya Sudan Kusini mwaka 2011. Tangu Desemba 19 mwaka 2018,…

Read More