Safari ya mwisho ya Annan Kesho.

Kesho Alhamisi ni siku ambayo mwili wa aliyekuwa Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan utazikwa pale Ghana na ni siku moja tu tangu uwasili ukitokea Uswizi ambapo alifariki akiwa huko. Annan ambaye ni mwafrika wa Kwanza kuongoza umoja wa mataifa alifariki dunia mnamo asubuhi ya tarehe 18 Mwezi August Mwaka huu pale Bern nchini Uswizi akiwa na umri wa miaka 80. Kwa sasa mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa siku ya kesho. Facebook Comments

Facebook Comments

Read More