Marekani imeweka vikwazo kwa raia wa Russia na makampuni kutoka Russia

Marekani imesema makampuni hayo yalijaribu kukwepa vikwazo katika mpango ambao unaweza kuondoa dola bilioni 1.5

Wizara ya fedha ya Marekani siku ya Jumanne iliweka vikwazo kwa raia mmoja wa Russia, na makampuni matatu yenye makao yake Russia ambayo ilisema yalikuwa yanajaribu kukwepa vikwazo vya Marekani katika mpango ambao unaweza kuwa umeondoa zaidi ya dola bilioni 1.5 za kampuni ya chuma ya mmiliki tajiri mkubwa wa Russia Oleg Deripaska.

Deripaska, mwenyewe aliwekwa chini ya vikwazo vya Marekani hapo Aprili 2018, aliingia katika biashara ya chuma wakati Umoja wa Sovieti ulipoanguka, na kupata utajiri kwa kununua hisa katika viwanda vya bati.

Forbes ili-orodhesha utajiri wake mwaka huu ni dola bilioni 2.8. Hazina ilisema kuwa Juni 2023 Deripaska alishirikiana na raia wa Russia, Dmitrii Beloglazov, mmiliki wa kampuni ya Obshchestvo S Ogranichennoi, inayotoa huduma za kifedha yenye makao yake Russia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii